Saturday 17 June 2017

Mambo 10 Yatakayo Tokea Endapo Cristiano Ronaldo Atarudi Manchester United

Editor: Evarist G.I


#1. Kuta kuwa na stori nyingi juu ya mahusiano mabovu yaliyokuwepo kati ya Ronaldo na Mourinho pale Real Madrid. Je safari hii wataweza kufanya kazi vizuri?

#2. Fargie atajihusisha zaidi na maswala ya timu pale tuu Ronaldo atakapo rudi Manchester United. Mchezaji bora kabisa katika maisha ya Babu Fargie usishangae kumuona akitaka kuwa karibu na mchezaji wake huyo kipenzi.


#3. Mashabiki wa Arsenal/Manchester City/Liverpool/ na Chelsea watatumia nguvu nyingi kuzungumzia umri wa Ronaldo kuwa ni mzee. Kwa imani yao watatamani ashindwe kucheza katika kiwango cha juu.

#4. Zlatan Ibrahimovic atasahaulika mapema sana.

#5. Antoine Griezman hatakua na maana tena klabuni Manchester United.


#6. Jezi namba 7 itafufuliwa katika kipindi muhimu ambacho Man U wanahitaji kurudi kwenye nafasi ya ubingwa na timu inayotisha zaidi duniani.


#7. Utakua ni mwisho wa maisha ya Rooney klabuni hapo, Wachezaji hawa nguli walikua katika hali ya sintofahamu pale ronaldo alipotaka Rooney atolewe kwa kadi nyekundu katika mechi ya kombe la dunia timu zao za taifa zilipokutana.


#8. Leo Messi atapata nafasi kubwa ya kuwa tena mchezaji bora wa dunia na hatakua na mpinzani hadi atakapo staafu. cr7 amekua akifunga goli nyingi ligi ya mabingwa Ulaya kila msimu lakini hatoweza kufanya hivyo akiwa na kikosi cha mashetani wekundu.


#9. Mashabiki na wapenzi wa Manchester City watataka Leo Messi ajiunge Man City.


#10. Mashabiki wa Arsenal Wataugua ghafla kwani mnyama wanae muogopa atakua amerudi jijini.


TOA MAONI HAPO CHINI
UNAHISI NINI KITATOKEA PALE CR7 ATAKAPO HAMA REALNA KWENDA MAN U?


credit: websources 

No comments:

Post a Comment