Saturday 24 June 2017

Misemo 10 Ya Jose Mourinho




Writer: SirgwajeTv

 THE SPECIAL ONE


 Jose Felix Mourinho kocha mbunifu,fundi na mwenye maneno mengi kama mzaramo wa Tanzania. Kocha wa zamani wa timu ya Chelsea, Porto, Inter Milan, Real Madrid na kocha wa mashetani wekundu kwa sasa.
Mourinho anasifika kwa maneno yake mengi ya kejeli kwa wapinzani wake hasa  kwa bwana Wenger wa Arsenal na wengine wengi, mwenye maneno ya kujisifia na mwenye kujitetea sana pale maji yanapozidi unga yani mambo yanapoenda kombo. 

Fuatilia kwa undani misemo 10 ya Mourinho kumbuka hii


"Mpira wa miguu ni mchezo unaohusu hisia na akili nyingi"

"Muda mwingine unaweza ukaona watu wazuri wasio na akili.
Muda mwingine unaweza ukaona watu wenye sura mbaya lakini wana akili
kama wanasayansi"
"Kitu pekee ambacho hatuwezi kudhibiti ni Mashabiki"
"Hua sipendi kuzungumzia kiwango cha mchezaji binafsi. Wachezaji hua hawashindi vikombe timu hushinda, kikosi hushinda vikombe"
"Ninapo kwenda kwenye chumba cha habari kabla ya mechi akilini mwangu mechi hua imeshaanza tayari"



"Jina langu ni Jose Mourinho na sibadiliki. Nilikuja na ubora wangu na mapungufu yangu"
"Kutokua na furaha ni neno zuri"
"Dunia imejaa ushindani, vurugu, matumizi mabaya,na ubinafsi. Kwa muda wote tuliopo hapa ni lazima tuzingatie yote"
"Nafurahia  kazi, nafurahia kila dakika ya taaluma katika maisha yangu"
"Ninawachezaji wa viwango vya juu, samahani tuna kocha wa kiwango cha juu. Tafadhali usiniite nina kiburi kwa hichi nitakacho kisema kwani ni ukweli. Mimi ni mshindi wa kombe la mabingwa ulaya, sipo nje ya chupa , lakini nadhani mimi ni mtu maalumu" 

COMMENT BELOW
AND 
SHARE!!!! 
 
Credit: Jose_Mou and Evarist G.

No comments:

Post a Comment