- Tafuta uwiano katika maisha yako.
- Fanya kazi kwa jitihada zako zote kila siku
- Kuwa wa kipekee
- Endelea kujifunza
- Dhihirisha wewe ni nani
- Jifunze kwa bidii
- Fanya kile ukipendacho
- Saidia wengine
- Endeleza urafiki mkubwa
- Fanya mambo kwa ubora
Jet Li - Siri 10 za Mafanikio
Maisha katika karne ya 21 si mepesi hata kidogo, watu wa kisasa wamekua wakichakarika muda wote na kumekua na changamoto nyingi. Maendeleo ya kiteknolojia yamekua yakifanya kila kitu kiwe cha haraka haraka simu zimekua za kasi, intaneti zimekua kasi na magari pia yamekua ya mwendo kasi. Kutokana na kasi ya maisha iliyopo inatulazimu kuongeza muda wa kufanya kazi kutoka muda wa masaa 8 hadi 16 kwa siku. Muda mwingine inatubidi hata tufanye kazi kwa masaa 21. Tukiwa tumechoka kabisa muda wa kulala bado tunapokea simu na kosama barua pepe ambazo tumetumiwa. Kitu cha kwanza tunapo amka asubuhi ni kuanza kuwasiliana kujua mambo yataendaje. Katika dunia hii ya mwendokasi na maisha ya kisasa tumekua tukivurugwa akili na kupata magonjwa mengi.
Katika tamaduni za watu wa kale wa China walikua wana mbinu nyepesi yenye busara: Weka uwiano, ishi maisha yako, kimbia kwa kasi kubwa katika hali ngumu muda wote kama vile unakimbizana na mchana na hautaki usiku ukufikie. Hatutakiwi tuishi kwa njia hiyo, badilisha mtazamo wako tembea kwa makini huku ukipunguza kasi hapo ndipo utakapo weza kupata uwiano....kutafuta uwiano katika maisha ni sehemu kubwa na muhimu kabisa.
Katika maisha yangu siku zote hua ninaamini adui mkubwa ni mimi mwenyewe. Tunatakiwa tupigane. Unajua watu wengi wamesha umia sana katika sanaa ya karate lakini tunatakiwa tupigane dhidi ya hali hiyo.
Kila siku tunatakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kuonyesha jitihada ya dhati kwa kadili ya uwezo wetu wote. Hivyo basi nadhani maana ya neno kutokua na uoga katika kichwa cha Jet Li ni kufanya kazi kwa bidii kila siku.
Mambo mabaya yanapo kutokea huna uwezo ya kuyadhibiti, yaache yaende, mambo mazuri yanaweza kutokea pia yaacha nayo yaende, hatujui mambo yatakayo tokea mbele hivyo hatuna budi kufanya kazi kwa nguvu zetu zote ili tuweze kufanikiwa katika maisha yetu.
Mimi sio Bruce Lee.Wala siwezi kamwe kua Bruce Lee. Alikua katika kizazi tofauti na hata filosofia tofauti. Vitu vingi vipo tofauti. Kila inadamu ameumbwa kipekee. Kila mtu anauwezo wa kipekee ni kazi kwako kuufanya huo uwezo uzae matunda. Kama unamfuata mtu kila siku basi utakua mfuasi na sio muanzishaji.
Mara nyingi hua najiambia mwenyewe sahau yaliyopita. Niliyoyafanya huko nyuma. hujiona kama mtu mpya, .kila siku vitu vipya hutokea. Natakiwa nijifunze Kiingereza. Natakiwa nijifunze vitu vipya ,natakiwa nijifunjze maisha ya Kimarekani. Muvi hii imefanikiwa lakini labda muvi ijayo haitafanikiwa. Hivyo basi unatakiwa ujifunze tena. Mimi ni muigizaji mpya kila siku. Hii ndiyo falsafa ya maisha yangu. Natakiwa nijifunze niweze kucheza nafasi mbalimbali. Kuna msemo mmoja wa kichina unasema unapozidi kua mzee unatakiwa uzidi kujifunza, uzee uzee uzee kujifunza kujifunza kujifunza zaidi.
Unatakiwa uthibitishe katika dunia ni jinsi gani unaweza kufanya vitu vizuri zaidi kuliko watu wengine. Hivyo basi unatakiwa ujithibitishe wewe ni nani, kimwili na kiakili. Siku zote unatakiwa ujithibitishe wewe ni nani hata kama unafanya vitu vipya, na kama unaweza kuonyesha kipaji chako, na ukajithibitisha, basi unauhakika wa kuwa na maisha ya mafanikio. Napenda kuamini kwamba Wachina au Wakanada kila watu wanatakiwa wafanye mambo yao tofauti. Hata wewe unao uwezo wa kujifunza mambo mapya kutoka katika jamii za watu wengine.
Nchini Marekani watu hujifunza kwa masaa 2 tuu kwa siku mara tatu kwa wiki, Nchini china wanafunzi hutumia zaidi ya masaa 8 kujifunza na ndio maana hufanya kazi kwa bidii zaidi.
Nakumbuka siku moja mwalimu alituambia tuweke mguu mmoja juu ukutani kwa muda wa masaa 4. Baada ya muda mfupi mwalimu alitoweka na hatukujua alipo elekea hivyo basi tuliendelea kuweka mguu juu na tuliogopa kuushusha kwasababu muda wowote ule mwalimu angeweza kurudi. Masaa 4 yalipotimia ndio ulikua mwisho wa mazoezi. Hivyo basi katika maisha ya kawaida ili tuweze kufanikiwa ni lazima tujue jinsi ya kujiendesha wenyewe.
Nadhani uwe umefanikiwa au hujafanikiwa siku zote ungependa kufanya jambo ambalo lingekufanya uwe na furaha. Sio tu kwasababu ya pesa au jina. Unatakiwa ufanye jambo ambalo kweli unalipenda kulifanya. Hisia ya kufanya jambo nilipendalo ni muhimu sana katika maisha yangu.
Kila siku hua nnafikiria jinsi ya kuwasaidia watu wengine duniani. Kwa upande wangu hufanya jitihada za kuwasaidia watu wengine sababu ni muhimu sana kwangu.
Binadamu wanaweza kuishi duniani kama familia kubwa, kuwa wamoja, familia moja. Japokua tunatofauti katika dini zetu, mifumo tofauti, lugha tofauti, rangi tofauti, lakini bado sisi ni binadamu tuu. Tunatakiwa tusaidiane kwa kila hali na sio Wachina wasaidiane wao kwa wao tuu. Tunatakiwa tusaidiane bila kujali itikadi zetu.
Jet Li ni mtu mwenye kuishi maisha ya siri. Nafikiri huficha kitu fulani. Yupo sawa kwasababu amekua pale kwa muda mrefu. Watu husema Jet Li ni mtu wa dini sana. Ukweli ni kwamba Jet Li ni mtu anayependa sana kujumuika na watu wengine na hujenga urafiki kwa sababu rafiki ndiye mtu wa kutoa msaada pale unapo kwama. Msemo wa wahenga wakiswahili husema akufaae kwa dhiki ndiye rafiki.
Siri#10: Fanya mambo kwa ubora
Katika kazi siku zoote hua nina amini ukifanya kazi katika ubora ndio matokeo mazuri huja. Hivyo basi jitahidi ufanya kazi kwa jitihada zako zote. Kizuri chajiuza kibaya cha jitembeza. Maana halisi ya kufanya kitu bora ni kukuwezesha kufikia malengo yenye mafanikio kwa muda mrefu.
Siri#10: Fanya mambo kwa ubora
Katika kazi siku zoote hua nina amini ukifanya kazi katika ubora ndio matokeo mazuri huja. Hivyo basi jitahidi ufanya kazi kwa jitihada zako zote. Kizuri chajiuza kibaya cha jitembeza. Maana halisi ya kufanya kitu bora ni kukuwezesha kufikia malengo yenye mafanikio kwa muda mrefu.
QUOTE!!!
THANKS FOR READING OUR SITE
PLEASE SHARE TO
INSIPRE THE WORLD!!!
Credit: Evarist G.I (Author), Jet Li na Wasomaji Wetu