Wednesday 14 June 2017

Wachezaji 10 Bora Katika Historia ya Manchester United

Writers: Evarist G.I & Allen H.B

Vigezo vilivyotumika katika kuchagua listi hii ni uwezo wa mchezaji kusakata kabumbu, mchango katika soka kwa ujumla, soko na biashara katika timu, tuzo binafsi, makombe mbali mbali na mapenzi ya mashabiki kwa mchezaji mmoja mmoja.

Ungana nami na usisahau kutoa maoni yako.


#10. Peter Schmeichel
Hata bomu la masafa marefu halikua na uwezo wa kumtungua golikipa bora katika historia ya dunia.
Golikipa mwenye rekodi nzuri ya kufunga magoli akicheza nafasi ya golikipa..... hii ni nouma!!!
Golikipa bora pamoja na Van Der Saar waliifanya ngome ya Man U kuwa ngumu na isiyofungika kiurahisi.
Kwa ufupi Schmeichel alikua kipa bora na bado ni bora katika historia ya Man U.

#9. Paul Scholes
Kiungo fundi aliyeifanya Man U iwe na kiungo bora nchini Uingereza. Paul na Giggs wamejitengenezea rekodi nyingi sana kwa kuchukua vikombe vingi.
Pasi ndefu, pasi fupifupifupi za maudhi na mtengenezaji bora kabisa wa pasi za mwisho na bila kusahau mashuti ya nguvu katika umbali wowote ule unamfanya Paul Scholes aingie katika kumi bora ya wachezaji bora kabisa katika historia ya Manchester United.

#8. Ruud Van Nesterooy
Mfungaji bora kabisa katika klabu ya Manchester United. 
Alikua na uwezo wa kufunga goli katika mazingira magumu na yasiyo tarajiwa.
Alikua akiitwa Van Magoli, nusu kosa umeumia.
The Goal Machine ndio neno pekee la kumsifia Mdachi huyu.

#7. David Beckham
Hakua machachari sana uwanjani kama wachezaji wengine, Mfungaji hatari wamipira iliyokufa.
Beckham aliweza kufanya mapinduzi katika historia ya mpira wa miguu
kutoka katika mchezo wa kulipwa na kua wa kibiashara. Bekham alikua ndiye mchezaji
aliyeongoza kwa mauzo ya jezi klabuni Man U na kuifanya kuingiza pesa ndefu,
Uwepo wa Bekham uliifanya Man U kushikilia nafasi ya Kwanza kama 
timu tajiri zaidi duniani.

#6. Eric Cantona
Eric "King"  Cantona mchezaji bora kuonekana katika klabu ya Man U. 
Msumbufu yeye, machachari yeye nk. aliifanya Man  U kurudi katika ubora wake.

#5. Sir Bobby Charlton 
Mchezaji anayeonekana kama mchezaji bora kabisa katika historia ya Man U,
alifanya mambo makubwa iliyopelekea kupewa heshima ya kuitwa SIR na 
Malkia wa Uingereza. Mchezaji huyu aliiweka Man U katika ramani ya dunia.

#4. George Best
Winga machachari  kuwahi kuonekana katika historia ya Man  U, fundi wa vyenga vya madowido na mwenye uwezo wa kufunga magoli ya aina zote.Kwa mtu anayejua soka atanielewa nikisema Best alikua mchezaji wa hadhi ya nje ya dunia hii.

#3. Wayne Rooney
Nduye mfungaji bora wa miaka yote katika historia ya Man U, wengi wangependa kujua ni kwanini asiwe ndiye mchezaji bora namba moja.
Rooney mchezaji aliyekua na kasi kama treni ya umeme.
Hakuwahi kuiangusha timu ya Mashetani wekundu.
Rooney ni kati ya Kapteni bora kabisa katika historia ya Manchester United.
Rooney ni kati ya Waingereza wachache walio dumu katika kiwango cha juu kwa zaidi ya muongo mmoja
yani miaka zaidi ya kumi.



#2. Cristiano Ronaldo
Winga machachari,
winga mwenye kasi ya ajabu,
winga asiyekabika,
winga aliyeshushwa toka mbinguni,
winga wa maajabu,
winga wa miujiza.
Jina lake ni Cristiano Dos Santos Aveiro Ronaldo, alisajiliwa akiwa kinda mdogo akiwa mbavu mbili mwepesi kama unyoya wa njiwa, dunia iliamini hatoweza kufanya mambo makubwa. Lakini chini ya usimamizi wa kocha Sir Alex Farguson, mtoto huyu ametoka katika kiwango cha kawaida na kuwa mtu si wakawaida.
Spidi, magoli ya aina zote, mipira iliyokufa, penalti inamfanya ronaldo kuchukua nafasi ya pili
kama mchezaji bora kabisa katika historia ya Man United.
CR7 ndiyemchezaji wa mwisho kujishinda tuzo ya Balon D'or 2009 hadi sasa
hakuna mchezaji kutoka ligi ya EPL aliyeshinda tuzo hizo.

#1. Ryan Giggs
Mchezaji bora kabisa katika historia ya Manchester Uniter ukipenda mwite Mugabe, ukipenda muite Mfalme wa Man U, ukipenda mwite Super Captain, nk. Mchezaji huyu toka akiwa kinda mdogo alionekana kuwa kiongozi bora.
Nguli namba moja klabuni Man u aliweza kuchukua mataji 13 ya ligi kuu ya Uingereza EPL, Ligi  ya Mabingwa Ulaya 2, FA 4, nk.


TOA MAONI YAKO 
UNADHANI NANI ALITAKIWA AWEPO NAYUPI ATOKE


Credit: ManU_tv, Banobi and Manutd.com

No comments:

Post a Comment