Sunday, 23 April 2017

Njia 5 za Asili za Kumaliza Upungufu wa Nguvu za Kiume

Author: TheActiveDreamer
"The patriot's blood is the seed of Freedom's tree."
~Thomas Campbell


Upungufu wa nguvu za kiume ni nini?
Tafiti zainaonyesha zaidi ya asilimia 50 ya wanaume wote duniani wenye umri kuanzia miaka 65+ wanasumbuliwa na tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume.

Maana: Ni hali inayojitokeza pale mwanaume anaposhindwa kusimamisha uume wake vizuri au  kushindwa kufanya tendo la ndoa kwa ufasaha. Dalili moja kuu ni ukosefu wa hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Hali zinaweza kumfanya mwanaume ashindwe kufanya tendo la ndoa kiufasaha ni pamoja na:
  • Uchovu
  • Kuchanganyikiwa
  • Maswala ya kimahusiano
  • Wasiwasi wa kufanya tendo la ndoa
  • Matumizi ya Pombe

VITU VINAVYO SABABISHA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Vitu vingi vinao uwezo wa kumfanya mwanaume ashindwe kufanya vizuri tendo la ndoa. Ili uume uweze kusimama vizuri  vyombo muhimu katika mwili huusika kama vile Ubongo, Homoni, Misuli, Neva na Mishipa ya Damu. Tatizo katika vyombo hivyo hapo juu huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.

Visababishi Muhimu
  • Magonjwa ya Moyo
  • Kisukari
  • Fetma
  • Matumizi ya Tumbaku
  • Ugonjwa wa Parkinson
  • Kuvimba kwa Tezi Dume


Njia 5 za Asili za Kuondoa Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume

Je, unauwezo wa kukimbia kwa mwendo wa kasi kama ulivyokua na umri wa miaka 20? Unauwezo wa kupiga mpira kwa umbali mrefu uwezavyo?

Labda huwezi tena.

#1. Anza Kutembea: Kwa mujibu wa utafiti uliofanya na chuo kikuu cha Harvard nchini Marekani unaonyesha mtu anayetembea kwa dakika 30 kila siku anapunguza athari ya kuweza kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume kwa zaidi ya asilimia 41% . Tafiti nyingine zinasema mazoezi ya kati yanaweza  kusaidia kuondoa upungufu wa nguvu za kiume kwa watu wenye umri wa kati.

#2. Kula Chakula Bora: Tafiti zilizafanywa huko Massachussets nchini Marekani unaonyesha watu wanao kula vyakula vya asili kama vile mboga za majani, matunda, karanga, na samaki hupunguza athari ya kuweza kupata tatizo la nguvu za kiume. Chagizo lingine upungufu wa vitamini B12 kwa muda mrefu huweza kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.

#3. Kua Makini na Afya ya Mishipa:  Shinikizo la damu, wingi wa sukari mwilini, wingi wa cholesterol, na wingi wa triglycerides vyote hivi husababisha uharibifu wa mishipa ya damu ya arteri inayosukuma damu kutoka kwenye moyo, kwenye ubongo, na kusababisha upungufu wa msukumo wa damu katika uume. Onana na daktari wako uone kama ni aina gani ya  mishipa ya damu ni dhaifu au imeathirika. Unataikiwa ubadilishe aina ya maisha unayoishi yanayoweza kusababisha upate athari za namna hii au ikiwezekana upate matibabu kwa daktari.

#4. Umbile ni  kitu Muhimu, kua mwembamba na ubakie hivyo:  Mtu mwenye kifua cha Inchi 45 anakua kwenye hatari zaidi ya kupata upungufu wa nguvu za kiume tofauti na mtu mwenye kifua cha kawaida cha inchi 32. Kupunguza uzito ni njia nzuri ya kuondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Obesity (Fetma) huwapata zaidi watu wenye uzito mkubwa. Ongozeko la mafuta mengi katika mwii wa binadamu hupelekea kupunguza ufanisi wa homoni katika mwili.

#5. Tembeza Msuli Wako: Ufanyishe mazoezi uume wako kwa kuubonyeza msuli wa vein ili mskukumo wa damu usiweze kupungua kwa haraka. Utafiti uliofanya huko Uingereza unaonyesha kuo mwanaume anayefanya mazoezi haya kwa muda wa miezi 2 mara mbili kwa siku  huweza kupunguza tatizo hili kwa kiasi kikubwa. Mazoezi haya ni pamoja na kubadilisha mtindo wa kimaisha kama vile kuacha kuvuta sigara na tumbaku, kupunguza uzito, na kuacha ulevi uliopindukia.

Kwa tatizo ambalo ni sugu zaidi wasiliana na daktari.

 SHARE AND COMMENT!!!

"FAIL AND WIN ARE BOTH RIGHT CHOICE"
E.T