Mchezo wa mpira wa miguu umekua maarufu zaidi kuliko mchezo mwingine wowote ule duniani. Watu wamekua wakijipatia pesa nyingi sana kupitia mchezo huu, huku wengine wakiamini kua timu zao ni kama sehemu ya dini zao. Lakini pamoja na umaarufu na upenzi wa mchezo huu bora zaidi duniani mashabiki na wapenzi wengi hawajui historia na baadhi ya mambo mengine mengi muhimu kuhusu soka.
Ungana nami moja kwa moja kujua mambo usiyo yajua au ungependa kuyajua zaidi.
#1. Nchi kutoka Ulaya zimefanikiwa kucheza fainali za World cup isipokua fainal ya mwaka 1930 na 1950 tu.
#2. Idadi ya magoli mengi kufungwa katika mechi moja ni 19-0. Stade Olympique de L'emyrne, timu katuka Madagascar iliamua kujifunga magoli yenyewe kuonyesha mgomo wao dhidi uwamuzi dhidi ya marefa katika mechi iliyopita ambao walionewa.
#3. Mchezaji wa kwanza mweusi kucheza soka la kulipwa alikua anaitwa Arthur Wharton mnamo miaka ya 1800.
#4. Pele ndiye mtu wa kwanza kuita soka ni mchezo mzuri (a beautful game).
#5. Wamarekani na Wakanada ndio huita mpira wa miguu soka.
#6. 1964 maamuzi ya refa yalileta vurugu zilizopelekea zaidi ya watu 300 kufa nchini Peru.
#7. ASEC Abidjan ya Cote d'Ivoire ilicheza mechi 108 bila kufungwa kati ya mwaka 1989 hadi 1994.
#8. Neil Armstrong alitaka kuupeleka mpira mwezini lakini NASA walikataa na kuita haitakua umarekani.
#9. Mpira wa miguu unaotumika katika soka la kimataifa umebaki katika ukubwa na ujazo uleule kwa zaidi ya miaka 120, ujazo wa inchi 120.
#10. Zaidi ya 80% ya mipira inayochezwa duniani hutengenezwa nchini Pakistani.
THANKS FOR READING MY PAGE
BE PART OF MY PAGE BY SHARING TO OTHERS
CREDIT: fifa.com.