Wednesday, 7 June 2017

Mambo 10 Usiyoyajua Kuhusu Nchi ya Indonesia

Author: TheActiveDream

Indonesia ni nchi iliyopo katika bara la Asia, nchi hii imeundwa kwa mkusanyiko w visiwa vingi sana. Kama ilivyo kwa kila nchi duniani Indonesia inavitu vyake adimu kabisa ambavyo ungependa kuvijua kwa ufupi na kwa umakini kabisa.
Ungana nami ujue mambo kumi kuhusu nchi ya Indonesia. 

#1.
Indonesia ni kisiwa kikubwa zaidi duniani, kimeundwa kwa jumla ya visiwa vidogo vidogo 13,000.

#2.
Joka(Dragon) ndiye mnyama nembo ya taifa ya  Indonesia.


#3.
Indonesia ndiyo nchi inayoongoza kwa ukataji wa miti zaidi duniani ikifuatiwa kwa ukaribu kabisa na nchi ya Brazil.

#4.
Indonesia ndiyo nchi yenye idadi kubwa kabisa ya waumini wa Kiislamu duniani.



#5.
Mtu wa kwanza kuishi nchini Indonesia alifika mnamo miaka 45,000 iliyopita.


#6.
Nchini Indonesia kuna volcano inayotoa rangi ya bluu. 


#7.
60% ya watu duniani huishi katika nchi ambazo adhabu ya kifo ni sheria, nchi kama China, India, Indonesia na USA.

#8.
Kabila la Minangkabau la Indonesia linaendeleza utamaduni wa wanawake kua juu ya wanaume, katika ndoa mme huchukuliwa kama amekopwa na mwanamke.


#9.
Wastani wa wanawake wa Bolivia, Indonesia na Guetemala ni wafupi  sana na unaweza ukawaweka kwenye kundi la mbilikimo.



#10.
Mwaka 2010 mtoto mdogo mwenye umri wa miaka 2 aitwaye Ardi Rizal alitikisa vyombo vya habari kwa tabia ya  uvutaji sigara 40 kwa siku. 


BONUS!!!
Indonesia ndiyo nchi inayoongoza kwa kuwa na watu wafupi zaidi duniani.

 
CREDIT: Encyclopedia, and google_picture.


THANKS FOR VISITING OUR SITE 
 SHARE
 AND
 COMMENT BELOW