Friday 2 June 2017

Mambo 10 Usiyoyajua Kuhusu Soka- Sehemu ya Kwanza

By theactivedream

Mchezo wa mpira wa miguu umekua maarufu zaidi kuliko mchezo mwingine wowote ule duniani. Watu wamekua wakijipatia pesa nyingi sana kupitia mchezo huu, huku wengine wakiamini kua timu zao ni kama sehemu ya dini zao. Lakini pamoja na umaarufu na upenzi wa mchezo huu bora zaidi duniani mashabiki na wapenzi wengi hawajui historia na baadhi ya mambo mengine mengi muhimu  kuhusu soka.

Ungana nami moja kwa moja kujua mambo usiyo yajua au ungependa kuyajua zaidi.

#1. Asili ya mpira wa miguu (soka) asili yake ni China miaka ya 476 KB.

#2. Mpira wa miguu ndio mchezo unaochezwa zaidi na kuangaliwa zaidi kuliko michezo mingine duniani.

#3. Mpira wa miguu ndio mchezo maarufu zaidi duniani. Fainali ya kombe la dunia huonwa na zaidi ya wapenzi na mashabiki bilioni moja ulimwenguni kote.

#4. Michuano mikubwa zaidi kufanyika ilitoa timu 5098. Michuano hiyo ilifanyika mwaka 1999 huko Bangkok katika ligi ya daraja la pili. Zaidi ya wachezaji 35000 walishiriki michuano hiyo.

#5. Idadi kubwa ya magoli kufungwa katika mechi moja kwenye ligi yalifungwa na Stephan Stanis (Mfaransa) alipokua akikipiga katika klabu ya Racing Club de Lens in Disemba 1942.

#6. Kwa ushahidi wa video goli lililofungwa mapema zaidi lilichukua muda wa sekunde 2.8 likifungwa na Ricardo Olivera (Uruguay) Disemba 1998.


#7. Wachezaji hawakutakiwa kuvaa jezi za wachezaji pinzani hadi sheria hiyo ilivyo badilishwa mnamo 1913.

#8. Wachezaji hukimbia umbali wa wastani wa kilomita 9.65 katika kila mechi.

#9. Mchezo wa kwanza kabisa wa kikapu (basketball) ulichezwa kwa kutumia mpira wa miguu.

#10. Klabu ya kwanza kabisa duniani ilikua ni English Sheffield Football Club ya Uingereza. 
Ilianzishwa mnamo 1857 Colonel Nathaniel Cresswick and Major William Priest, wawili hawa walikua ni maafisa wa jeshi la Uingereza.

Credit: soccer.com, fifa.com, wikipedia, and goal.com/fn


TOA MAONI YAKO HAPO CHINI
MSHIRIKISHE MWENZAKO

SEHEMU YA 2 ITAENDELEA.......