Saturday 10 June 2017

Sababu 5 za Kifo cha Muammar Gaddafi Zimefahamika

Author: theHeroTv



Gaddafi hakuuawa kwa sababu za kiubinadamu, lakini ni kwasababu za mafuta na hela. Wazo lake la kuifanya Africa iwe na fedha moja ya dhahabu ilikua ni sababu moja kuu.

Barua pepe ya siri ya Hilary Clinton iliyodukuliwa imeonyesha madudu mengi na Africa ikihusika. Wikileaks waliiachia taarifa za siri za idara ya Marekani ambayo haikuwekwa wazi aliyotumiwa Clinton mnamo April 2 2011. Mtumaji wa barua pepe hiyo bwana Sidney Blumenthal alithibitisha kwamba dunia tayari imeshafahamu ukweli juu ya kifo cha Gaddafi kwamba ni maswala ya mafuta na fedha.

Mnamo Aprili 2011, Rais wa benki ya dunia, Robert Bruce Zoellick alizungumza kwenye mkutano kwamba ni jinsi gani anayo imani juu ya benki ya dunia kuwa itafanya juu chini kuutengeneza uchumi wa Libya katika hali nzuri kutokana na athari ya vita vya kumg'oa madarakani Hayati Gaddafi.  

Akasema "Ujenzi mpya kwa sasa ni Ivory Coast, Sudan \Kusini, Sri lanka, Liberia na nadhani hivi karibuni itakua Libya tuu".

Kwa mtu wa kawaida, hii ndiyo benki ya dunia ambayo tulikua tunaimani kwamba itakuja na ufumbuzi juu ya matatizo yanayotokea katika nchi ambaozo uchumi wake umeteteleka. Lakini kwa mchumi John Perkins
anasema Benki ya dunia haijapewa mamlaka ya lazima kutatua kila tatizo linalo tokea katika dunia. Kiukweli hii kauli imekaa sawa embu angalia Benki Kuu ya Marekani pamoja na ndugu yake IMF. USA anaudhibiti wa asilimia 16% wa benki ya dunia, wakati mtu wa pili kwa udhibiti ni Japani ambaye anaasilimia 7%. Pia Marekani inauhuru wa kupiga kura ya turufu ya asilimia 17% IMF.

Sasa tunaweza tukajiuliza endapo ikitokea nchi ambayo sio aminifu ambayo inauwezo wa kuleta mabadiliko ya kibenki yenye uwezo wa kuinufaisha nchi husika na kuzifanya IMF na Benki kuu ya dunia kupiga magoti kuziomba msaada? Nchi za Magharibi zina umoja wao uiitwao NATO ambao kazi yake kubwa ni kutumia mabavu kuzilinda nchi hizo na maslahi yao na kuzigandamiza nchi nyinginne.

Libya haikua aminifu, lakini swali ni maono gani ambayo Gaddafi alikua nayo kwenye kichwa chake?

Kwa mujibu wa IMF Libya ni nchi huru kwa 100% hadi mwaka 2011. Libya ilikua na tani 144 ya dhahabu katika benki yake. Gaddafi aliamini kua ataungwa mkono na nchi za Africa na nchi za Kiislamu katika mchakato wake wa kuifanya Africa iwe na Fedha moja yenye uwezo wa kupambana na Dolla ya Marekani, Yuro ya Ulaya na Paundi ya Uingereza.

Sababu hizi ndizo zilizomfanya Nicolas Sarkozy atengeneze hila za kumuua Gaddafi ni hizi Zifuatazo:

#1. Hamu ya kutaka apawe sehemu kubwa ya mafuta yanayozalishwa nchini Libya.
#2. Kuongeza ushawishi wa Ufaransa Kaskazini mwa Africa.
#3. Kuboresha nafasi yake ya uongozi   wa ndani nchini Ufaransa.
#4. Kuliweka jeshi la Ufaransa katika nafasi ya kiutawala duniani.
#5. Kuifanya nchi ya Ufaransa kuwa taifa lenye nguvu zaidi kaskazini mwa bara la Africa (Francfone Africa).

Kama Gaddafi angefanikiwa kuifanya sarafu moja ya umoja wa Africa, nchi ya USA na Umoja wa Ulaya zingekuja kununua madini kwa thamni ya pesa ya Africa.  


THANK YOU FOR  VISITING OUR SITE

Credit: Tatenda, Gaddafi Biography, and google images