Monday 6 March 2017

Washambuliaji 10 Bora Chini ya Utawala Wa Wenger, Giroud anachukua namba ngapi?

By  LivingDream


Leo  tunaangali  washambuliaji 10 bora katika utawala wa Arsene  Wenger  je,  Oliver  Giroud  anasi mama nafasi ya  ngapi?



10. Emmanuel Adebayor

Msambulaiji  aliyechukiwa  na  mashabiki wa arsenal  baada ya kuifunga  timu yake ya  zamani kushangili kama  mbwa  kichaa.  Lakini  wapenzi wa  Arsenal  watabaki kumkumbuka kwa  uwezo wake wa kufun ga goli  alipokua akiwatumika.

9.  Wiltord

Mshambuliaji  aliyefunga goli  la ushindi  pale  Old  Traford  na mchezaji aliyeshiriki  kuisaida  Arsanal  kushinda vikombe kadha  wa kadha.  Japokua  alilikua  mfungaji  mzuri l;akini  hakuweza  kuteka  hisia  za  mashabiki wa Asenal  kutokana  na  kukosa goli  nyingi  na  zakizembe.
8.  Eduardo
Mshambuliaji aliyeonekana kama msaada mkubwa uliopatikana  na Arsene Wenger,  kila   mtu  aliamini kua Eduardo atakuja kutisha sana  kama sio  ajali  mbaya aliyoipta  katika  mechi  shi ya  Birmingham  alipovunjika  mguu.  Toka  hapo Eduardo  hakuweza kurejea  katika  kiwango chake  cha  kawaida.

7.  Nwankwo  Kanu
Mchezaji  aliye tia  mguu  uwanjani akikimbia pale alipojiunga na  Arsenal,  japokua  Kanu  hakuweza  kufikia  malengo  ambayo wengi walitarajia  lakini  anabaki kua  mshambuliaji   bora  katika utawala wa  Wenger  kwa  miaka  mingi ijayo.

6.  Nicolas Anelka


Kijana aliyeonekana kua bora sana alisajiliwa na  Arsene Wenger,  aliweza  kutikisa  klabuni hapo kwa  muda  mfupi na  baadae akaamua  kutimkia  klabu ya Real Madrid ya Spain.  Toka alipohama  Arsenal hakuwez a kurejesha kiwango  chake  hadi alipostaafu,  mashabiki  na wapenzi wa Arsenal hawakulaumu sana kwani pesa zilizotumika kumuuza waliweza k ununua  wachezaji wengine bora.

5.  Oliver  Giroud
Mshambuliaji  anaeendela  kukukua, japo mashabiki na wapenzi  wengi  wa Arsenal  hawampi sifa  anazostahili lakini anabaki kua  mshabuliaji  bora.

4.  Robin Van  Persie

Mtu  anayechukiwa  na  mashabiki wa  Arsenal  kwa kitendo chake cha kuhamia katika  klabu  pinzani zaidi ya  Manchester United.  Lakini  Van  Persie  atakumbukwa  na  wapenzi wengi wa  Arsenal  kwa  magoli yake ya  mguu  wa kushoto yaliyowapa raha.
 
3.  Ian  Wright
  Alikua  ameshaanza kushuka kiwango pale  Wenger alipochukua  madaraka Arsenal  lakini bado alikua  mtu muhimu aliyeisaidia   Arsenal kuchuku vikombe 2 mfululizo  1997/8.  Ian  alikua  mshambuliaji  bora wa  Arsenal kwa kipindi hicho.

 
2.  Dennis  Bergkamp

 Hakua  mshambuliaji moja kwa moja,  lakini aliweza kuifungia Arsenal goli 100 na  kutengeneza   mfumo ambao  kila  mshambuliaji aliyecheza  naye aliweza kufanya  vyema kutokana na uwepo wa  Bergkamp.  Alikua  akiitwa  ndiye  mungu wa  Arsenal.


1.  Thiery  Henry

Hawezi kua  mtu  mwingine yeyote  zaidi  ya huyu  mtu.  Thiery Henry  ndiye  mshambuliaji  bora  zaidi katika historia ya klabu ya Arsenal  kwa  kufunga  goli  228  nakuifanya Arsenal kua timu inayotisha zaidi na  kuweza kumaliza  msimu wa 2003/2004 kushinda ligi  bila kufungwa  hata  mechi  moja.

TOA   MAONI  YAKO  UANONA  NANI  AMEPENDELEWA?
NANI ATOKE  NA  AINGIE  NANI?
SHARE  TO  YOUR FRIENDS!!!!
Author:  Alen  H.  and Evarist G.
Sources: www.arsenalfc.com
 

1 comment:

  1. Japokuwa hawi top scorer lakini ananakua miongoni mwa top scorers.

    ReplyDelete