Kwa wale wasiomjua Buffet ni kibabu ambaye amekua kwenye GAME ya ujasiriamali kwa muda wa miaka mingi sana.
Amekua akichaguliwa kama mtu tajiri zaidi duniani mara kadhaa, jarida la Time Magazine lilimchagua kama mtu mwenye mchango zaidi duniani; anatajwa kama mwekezaji bora zaidi katika karne ya 20 na 21.
Warren Buffet aliyezaliwa Agosti 30 1930 (86) ni Mwekezaji na mtoa misaada ni raia wa Marekani mwenye utajiri wa dola za kimarekani $78.7 billion (sawa na tzs 175,893,435,844,713.00).
Kwa ufupi kabisa Warren Buffet ni BOSI.
HIZI NDIZO SIRI 10 ZA MAFINIKIO ALILIZITUMIA WARREN BUFFET"Price is what you pay. Value is what you get."
Buffet
Siri#1: Wekeza Faida Yako
Unapopata pesa kishawishi cha kuzitumia hua ni kubwa sana. Kuliko kuzitumia pesa njia sahihi ni kuiwekeza faida yako. Buffet alijifunza hii njia akiwa na umri mdogo kabisa, alipokua shuleni yeye na rafiki yake walinunua pinball machine na kuiweka katika ofisi ya kunyolea nywele. Waliupokua wanapata pesa zaidi walizidi kununua mashine nyingine hadi wakafanikiwa kua na ofisi 8. Rafiki zake walipo kua wanauza miradi yao Buffet aliwekeza katika mifuko ya kijamii na kufungua miradi mingine zaidi.
Siri#2: Kuwa Tayari Kuwa Tofauti
Usiweke maumuzi yako kwa kuwaridhisha wengine, watakuonaje na wasemaje. Buffet alipoonza kusimamia pesa mwaka 1956 alikua na kitita cha dola za Kimarekani 100,000 alifanya kazi Omaha na sio katika kuta mitaa mbalimbali. Siku zote alikataa kuwaambia wenzake ni wapi alikua anatunza pesa zake. Watu wengi waliamini kuwa ni lazima tuu ashindwe lakini baada ya miaka 14 baadae ya ushirika Buffet alikua na kitita cha $100m.
Siri#3: Kamwe Usinyonye Kidole Chako
Hakikisha unatafuta taarifa kwa undani iliziweze kukusaidia kufanya maamuzi, na hakikisha unawauliza marafiki zako au mpenzi wako kama kweli bado upo kwenye mstari. Buffet hujisifia kwa maamuzi yake ambayo huyafanya na huyasimamia. Epuka kupata muda wa kupoteza na kuanza kunyonya kidole.
Siri#4: Andika Mpango Wako kwanza Kabla ya Kuingia Mkataba
Mpango wako kwanza kabla ya kuanza kazi ni muhimu kabla ya kuanza kazi. hasa pale unapokua na kitu cha kutoa huku mwenzako pia anao uwezo. Buffet alijifunza hii mbinu kwa ugumu toka alipokua mdogo pale babu yake Ernest alipomuajiri. Alikua akiondoa barafu zilizo kua zimeganda eneo la biashara kwa muda wa masaa 5 hadi pale mikono ilivyo kakamaa kwa ubaridi na mwisho wa siku alikua akipewa kiasi cha senti 90 tuu za kimarekani.
Siri#5: Angalia Gharama Ndogo
Buffet anamiliki biashra zinazosimamiwa na mameneja ambao hujizingatia kiasi kidogo sana cha hasara. Kunakipindi alimuajiri mtu wa kuhesabu toileti paper 500 kila siku kuhaikikisha kama amedanganywa au la. Pia huthamini zaidi rafiki yule ambaye hupiga rangi nyumba ya biashara upande mmoja unaoshahibiana na barabara.
Related Post: Siri 10 za Mafanikio Ya Paul Walker
Siri#6: Kopa Kwa Kiasi
Buffet hakuwahi kukopa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya kuwekeza au kujengea nyumba. Hupokea barua nyingi sana za watu wakijaaribu kuzungumzia jinsi gani mikopo yao inaweza kua ya kimafanikio lakini mwisho wa siku huangukia katika madeni mazito. Ushari: Jadiliana na mkopeshaji wako kamauanweza ukamlipa kwa uwezo utakao kua nao. Napale unapokua huru dhidi ya madeni basi tuza faida yako kwa ajili ya uwekezaji wa baadae.
Kwa uvumilivu na dhamira ya kweli utakua na uwezo wa kushinda na wapinzani wako. Buffet alimiliki Nebraska Furniture Mart mnamo 1983 aliipenda kwa sababu mmiliki Rose Blumkin alivyokua akiendesha biasha vizuri. Muuhamiaji wa kutoka Russia alinzisha pawnshop na kuja kua na biashara kubwa ya mbao kubwa zaidi barani America Kaskazini. Siri yake ya mchezo ilikua ni kuuza vitu kwa bei ya chini kwa wingi sana na alikua bingwa wa kufanya wa kufanya mazungumzo.
Mara moja Buffet alipokua mdogo alienda kwenye mashindano ya kuendesha magari. Alicheza kamari na akashindwa. Ili aweze kurudisha pesa zake alizopoteza Buffet alicheza kamari tena na akashindwa tena. Alijihisi kuumwa karibu wiki nzimalakini alijifunza kosa lake na hakurudia tena.
Siri#9: Tathmini Athari
Mwaka 1995 mfanyakazi wa Buffet ambaye ni m toto wake alishutumiwa kuhusika na uhalifu wa kifedha na FBI. Buffet alimshauri Howie kwa kujaaribu kumpa mitazamo hasi ambayo ingeweza kutokea endapo tu angeendelea kubaki pale kazini ni jinsi gani angeweza kuathiri kampuni. Siku iliyofuata asubuhi Howie aliacha kazi.
Siri#10: Jua Maana Halisi Ya Mafanikio
Pamoja na utajiri woote wa Buffet lakini hua hapimi kipimo cha mafanikio kwa kigezo cha Dola. Mwaka 2006 alitaka atoe utajiri wake wote kwa wasio jiweza kwa njia ya misaada. Anaamini unapokua na umri kama wake kipimo sahihi cha mafanikio ni jinsi gani umeishi hapa duniani na kuwafanyawatu wenguine wawe na furaha kutokana na uwepo wako hapa duniani.
TOA MAONI YAKO CHINI HAPO
NI SIRI GANI ULIO IPENDA ZAIDI?
Authors: Evarist G., LivingDream and theactivedream
Credit & Sources: Wikipedia.com and Fobres.com
je naomba ushauri : nawezaje kukuza mtaji wangu kutoka kima kidogo hadi kuwa mfanya biashara mkubwa
ReplyDeletenahitaji ushauri kwa hili au mbinu