Monday, 6 March 2017

Siri 10 za Mafanikio Ya Warren Buffet

By  LivingDream

Kwa  wale wasiomjua  Buffet  ni  kibabu  ambaye  amekua kwenye GAME  ya  ujasiriamali kwa muda wa  miaka  mingi sana.  

Amekua  akichaguliwa  kama  mtu  tajiri zaidi duniani  mara kadhaa,  jarida la Time  Magazine lilimchagua kama mtu mwenye mchango zaidi duniani;  anatajwa kama mwekezaji  bora zaidi  katika  karne ya 20 na  21.
Warren Buffet aliyezaliwa  Agosti 30 1930 (86)  ni  Mwekezaji  na mtoa  misaada  ni raia wa Marekani  mwenye utajiri wa dola  za kimarekani  $78.7 billion  (sawa na tzs 175,893,435,844,713.00).

Kwa ufupi  kabisa Warren  Buffet  ni  BOSI.


"Price is what you pay. Value is what you get.
                             Buffet
HIZI NDIZO SIRI 10 ZA MAFINIKIO ALILIZITUMIA WARREN  BUFFET

Siri#1:  Wekeza Faida  Yako

Unapopata  pesa kishawishi cha kuzitumia hua  ni kubwa sana. Kuliko kuzitumia pesa njia sahihi  ni  kuiwekeza faida yako.  Buffet alijifunza  hii  njia akiwa  na umri  mdogo kabisa,  alipokua shuleni yeye  na rafiki yake walinunua pinball machine  na kuiweka  katika ofisi ya kunyolea  nywele.  Waliupokua wanapata pesa zaidi walizidi kununua  mashine nyingine  hadi wakafanikiwa  kua  na ofisi  8.  Rafiki zake walipo kua wanauza miradi yao Buffet aliwekeza katika mifuko  ya kijamii  na kufungua  miradi  mingine zaidi.

 
Siri#2:  Kuwa  Tayari Kuwa Tofauti

Usiweke  maumuzi yako  kwa  kuwaridhisha wengine,  watakuonaje  na wasemaje.  Buffet  alipoonza kusimamia  pesa  mwaka 1956 alikua  na  kitita  cha dola  za  Kimarekani  100,000   alifanya kazi Omaha  na sio  katika kuta  mitaa mbalimbali.  Siku  zote  alikataa kuwaambia  wenzake  ni wapi alikua  anatunza pesa zake.  Watu wengi waliamini kuwa  ni lazima tuu  ashindwe lakini  baada ya miaka 14 baadae ya  ushirika Buffet alikua  na kitita cha $100m.

 Siri#3:  Kamwe Usinyonye Kidole Chako
Hakikisha unatafuta taarifa kwa undani iliziweze kukusaidia kufanya maamuzi, na  hakikisha unawauliza  marafiki zako au  mpenzi wako kama kweli  bado upo   kwenye mstari.  Buffet hujisifia kwa  maamuzi yake  ambayo  huyafanya  na huyasimamia. Epuka kupata muda wa kupoteza  na kuanza kunyonya kidole.

Siri#4:  Andika Mpango Wako kwanza  Kabla ya  Kuingia  Mkataba
Mpango wako kwanza  kabla ya kuanza kazi  ni    muhimu kabla ya kuanza kazi.  hasa  pale  unapokua  na  kitu cha kutoa  huku  mwenzako pia  anao uwezo.   Buffet  alijifunza  hii  mbinu  kwa ugumu toka alipokua mdogo  pale babu yake Ernest alipomuajiri.  Alikua akiondoa barafu zilizo kua zimeganda eneo  la  biashara kwa  muda wa masaa 5 hadi pale  mikono ilivyo kakamaa  kwa  ubaridi  na mwisho wa siku  alikua akipewa  kiasi cha senti 90 tuu za  kimarekani.

Siri#5:  Angalia Gharama  Ndogo
Buffet anamiliki  biashra zinazosimamiwa  na  mameneja  ambao  hujizingatia  kiasi  kidogo sana  cha  hasara.  Kunakipindi alimuajiri  mtu wa  kuhesabu  toileti paper 500  kila  siku  kuhaikikisha  kama  amedanganywa au  la.  Pia huthamini zaidi rafiki yule ambaye hupiga rangi  nyumba ya  biashara upande mmoja unaoshahibiana na barabara.

Related  Post:  Siri 10  za  Mafanikio Ya  Paul Walker

Siri#6:  Kopa  Kwa Kiasi
Buffet  hakuwahi kukopa  kiasi kikubwa  cha  pesa  kwa  ajili  ya  kuwekeza  au  kujengea  nyumba.  Hupokea barua  nyingi sana  za watu wakijaaribu  kuzungumzia  jinsi gani mikopo yao inaweza kua ya kimafanikio lakini mwisho wa siku  huangukia katika  madeni  mazito. Ushari:  Jadiliana na  mkopeshaji  wako  kamauanweza ukamlipa  kwa  uwezo  utakao  kua nao. Napale unapokua huru  dhidi ya  madeni basi  tuza faida yako kwa ajili  ya uwekezaji wa  baadae.

Siri#7:  Kua  Mvumilivu
Kwa  uvumilivu  na dhamira ya kweli  utakua  na uwezo wa kushinda na wapinzani wako. Buffet alimiliki Nebraska Furniture Mart mnamo 1983 aliipenda  kwa sababu mmiliki  Rose Blumkin alivyokua akiendesha  biasha vizuri.  Muuhamiaji  wa kutoka Russia  alinzisha  pawnshop  na kuja kua  na biashara kubwa ya mbao  kubwa  zaidi  barani America  Kaskazini.  Siri yake ya  mchezo ilikua  ni kuuza vitu kwa  bei ya chini kwa  wingi  sana  na  alikua  bingwa wa  kufanya wa kufanya mazungumzo.

 Siri#8:  Jua Muda Sahihi  Wa Kuacha
Mara moja Buffet alipokua  mdogo alienda kwenye  mashindano ya kuendesha  magari.  Alicheza  kamari  na  akashindwa.  Ili  aweze  kurudisha  pesa  zake  alizopoteza  Buffet alicheza kamari tena na akashindwa tena.  Alijihisi    kuumwa  karibu wiki  nzimalakini alijifunza kosa lake na hakurudia  tena.

Siri#9:  Tathmini Athari
Mwaka  1995  mfanyakazi wa Buffet ambaye  ni m toto wake alishutumiwa  kuhusika  na  uhalifu wa kifedha  na FBI.  Buffet alimshauri Howie kwa  kujaaribu  kumpa mitazamo hasi  ambayo ingeweza kutokea  endapo tu angeendelea  kubaki pale kazini  ni  jinsi  gani  angeweza kuathiri kampuni. Siku iliyofuata asubuhi Howie aliacha kazi.

Siri#10:  Jua Maana Halisi Ya  Mafanikio
Pamoja na  utajiri  woote  wa Buffet  lakini hua  hapimi  kipimo cha mafanikio kwa  kigezo cha Dola.  Mwaka  2006  alitaka  atoe  utajiri  wake  wote  kwa  wasio  jiweza   kwa  njia  ya  misaada.  Anaamini unapokua  na umri kama wake kipimo sahihi  cha mafanikio  ni jinsi  gani umeishi  hapa duniani  na kuwafanyawatu wenguine wawe  na furaha  kutokana  na uwepo wako  hapa duniani.  

TOA  MAONI  YAKO  CHINI  HAPO
NI SIRI  GANI  ULIO  IPENDA ZAIDI?

Authors:  Evarist  G., LivingDream  and  theactivedream  
Credit &  Sources: Wikipedia.com  and Fobres.com

1 comment:

  1. je naomba ushauri : nawezaje kukuza mtaji wangu kutoka kima kidogo hadi kuwa mfanya biashara mkubwa


    nahitaji ushauri kwa hili au mbinu

    ReplyDelete