Barcelona,Arsenal na Napoli na timu nyingine je zitaweza kufuzu kwa hatua ya robo fainali ya klabu bingwa barani Ulaya 2016/2017? Ni swali ambalo mashabiki na wapenzi wa soka duniani wanajiuliza kama inawezekana, basi ungana nami hatua kwa hatua kujikumbusha maajabu yaliyofanywa na timu kadha walioweza kushinda goli nyingi na kuenda hatua ya robo finali.
FC Barcelona 5-1 Chelsea FC
1999/2000 quater finals
Chelsea kabla ya ujio wa Roman Abramovic, Chelsea haikua timu yenye nguvu barani ulaya kama ilivyo sasa. Barcelona chini ya Luis Van Gaal waliweza kupoteza mechi kwa kufungwa goli 3-1 dhidi ya timu ya Gianluca Vialli. Lakini ngwe ya pili Barcelona waliibamiza Chelsea kipigo kikali cha goli 5-1.
AC Milan 4-1 RC Deportivo La Coruña
RC Deportivo La Coruña 4-0 AC Milan
2003/04 quarter-finals
Walter Pandiani aliipa goli Depor walipokua Sansiro lakini hadi mechi inakwisha mambo hayakua mazuri kwa Depor kwani Ricardo Kaka alipiga goli 2 kati ya goli 4 za AC Milan. Wakati wa mahojiano kocha wa Depor Javier Irureta alisema kufuzu hatua ya robo ni ndoto isiyoelezeka lakini anaamini katika miujiza kwenye soka. Hadi inafika mapumziko Depor walikua mbele kwa magoli 3 kwa bila dhidi ya AC Milan, goli za Pandiani, Juan Carlos Valerón na Alberto Luque na mchezaji aliyeingia kipindi cha pili Fran González alifunga goli dakika ya 76. Deportivo waliondolewa katika hatua ya nusu finali.
Real Madrid CF 4-2 AS Monaco FC
AS Monaco FC 3-1 Real Madrid CF
2003/04 quarter-finals
Santiago Bernabéu on 24 March 2004 katika dakika ya 83 goli la Fernando Morientes liliipa AS Monaco matumaini ya kufuzu raundi ijayo. Kocha wa Monaco Didier Deschamps hakutaka kukata tamaa na kuwaambia waandishi wa habari kua kama ameshatolewa ni bora aende kulala nyumbani. Goli za Ludovic Giuly 2 na Morientes. Siku ya kufa nyani miti yote huteleza ni baada ya Raul Gonzalez kukosa nafasi ya wazi kabisa kwa kugongesha mwamba hakika ilikua ni nafasi muhimu sana ambayo ingebadilisha matokeo.
SSC Napoli 3-1 Chelsea FC
Chelsea FC 4-1 SSC Napoli (aet)
2011/12 round of 16
Mabadiliko ya kocha wa Chelsea AVB iliifanya chelsea kushindwa kufurukuta ilipoenda Italy lakini goli la Juan Mata liliipa Chelsea matumaini huku Napoli wakipiga goli kupitia Cavani 1 na Lavezi 2. Ujio wa kocha mpya Robert Di Mateo uliipa nguvu mpya clabu yachelsea nakuifanya iizabue magoli 4-1 Napoli pale ilipoenda darajani Stamford Bridge goli za Didier Drogba, John Terry na Frank Lampard.
AC Milan 2-0 FC Barcelona
FC Barcelona 4-0 AC Milan
2012/13 round of 16
Hakuna timu ambayo imewahi kushinda mechi ya kwanza 2-0 alafu ikashindwa kujipatia angalau goli moja la ugenini, lakini Barcelona ilifanya kweli pale ilipokub ali kipigo cha goli 2-0 pale Sansiro na kuweza kushinda goli 4-0.
Olympiacos FC 2-0 Manchester United FC
Manchester United FC 3-0 Olympiacos FC
2013/14 round of 16
Hamasa ya Sir Alex Ferguson ilisaidia kuwapa wachezaji wake nguvu ya ajabu pale walipo kubali goli 2-0 dhidi ya Olimpiacos FC na kuweza kushinda goli 3-0, goli za Robin Van Persie 2 na Joel Campbell.
Kipigo hicho kiliidhoofisha Olimpiacos na kuondoa ndoto yake kwenda hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza.
Paris Saint-Germain 3-1 Chelsea FC
Chelsea FC 2-0 Paris Saint-Germain
2013/14 quarter-finals
Chelsea kwa mara nyingine tena lakini kipindi hichi ilikua chini ya Jose Mourinho ni pale ngwe ya kwanza Chelsea ilipofungwa goli 3-1 goli moja lakujifunga la David Luiz na goli la dakika ya 93 la David Luiz. Ngwe ya pili goli la penalti la Eden Hazard na baadae mchezaji aliye ingia kutokea bechi Demba Ba alifunga goli la ushindi lililoiwezesha Chelsea kufuzu kwa hatua ya robo final.
Bonus Comeback
FC Porto 3-1 FC Bayern München
FC Bayern München 6-1 FC Porto
2014/15 quarter-finals
TOA MAONI YAKO KWA KUKOMENTI CHINI HAPO!!
No comments:
Post a Comment