Sunday 5 March 2017

Je Barcelona na Arsenal wataingia Robo Finali UCL 2016/17?

By LivingDream
Barcelona,Arsenal  na Napoli na timu  nyingine je  zitaweza  kufuzu  kwa  hatua  ya  robo fainali  ya  klabu bingwa  barani Ulaya  2016/2017? Ni  swali  ambalo  mashabiki  na wapenzi wa soka duniani  wanajiuliza kama inawezekana,  basi ungana   nami  hatua kwa hatua  kujikumbusha  maajabu  yaliyofanywa na timu  kadha  walioweza  kushinda goli nyingi na kuenda hatua ya  robo  finali.

Chelsea FC  3-1 FC Barcelona 
FC Barcelona  5-1  Chelsea  FC 
 1999/2000  quater finals
Chelsea kabla ya  ujio wa  Roman  AbramovicChelsea haikua  timu  yenye  nguvu  barani ulaya kama ilivyo sasa.  Barcelona  chini  ya  Luis  Van  Gaal  waliweza kupoteza mechi kwa kufungwa  goli  3-1 dhidi  ya timu ya   Gianluca Vialli. Lakini ngwe ya pili Barcelona waliibamiza  Chelsea kipigo kikali  cha goli 5-1.

AC  Milan 4-1  RC Deportivo La Coruña
RC Deportivo La Coruña 4-0 AC  Milan
 2003/04 quarter-finals
Walter  Pandiani  aliipa goli  Depor walipokua  Sansiro  lakini  hadi  mechi inakwisha mambo  hayakua  mazuri kwa Depor  kwani Ricardo Kaka alipiga goli  2  kati  ya goli  4 za  AC Milan.  Wakati wa mahojiano kocha wa Depor  Javier Irureta  alisema kufuzu  hatua ya robo ni  ndoto isiyoelezeka  lakini  anaamini  katika miujiza kwenye soka.  Hadi inafika mapumziko Depor walikua mbele kwa magoli 3 kwa  bila dhidi  ya AC Milan,  goli  za  Pandiani, Juan Carlos Valerón na Alberto Luque na mchezaji aliyeingia kipindi  cha pili  Fran González  alifunga goli  dakika  ya 76.  Deportivo  waliondolewa katika hatua ya   nusu finali.

 
Real Madrid CF 4-2 AS Monaco FC
AS Monaco FC  3-1 Real Madrid CF 
2003/04 quarter-finals
Santiago Bernabéu on 24 March 2004 katika  dakika ya 83  goli  la  Fernando  Morientes  liliipa  AS Monaco  matumaini  ya  kufuzu  raundi ijayo. Kocha  wa  Monaco Didier Deschamps  hakutaka kukata tamaa na kuwaambia waandishi wa habari kua kama ameshatolewa ni bora  aende  kulala  nyumbani.  Goli  za  Ludovic Giuly 2 na  MorientesSiku  ya kufa  nyani miti yote  huteleza ni baada ya   Raul  Gonzalez  kukosa nafasi ya wazi kabisa  kwa  kugongesha  mwamba  hakika ilikua  ni  nafasi  muhimu sana ambayo ingebadilisha  matokeo.
 

SSC Napoli 3-1 Chelsea FC
Chelsea FC 4-1 SSC Napoli (aet)

2011/12 round of 16
Mabadiliko  ya kocha wa Chelsea  AVB  iliifanya chelsea kushindwa kufurukuta ilipoenda Italy  lakini goli la Juan Mata liliipa  Chelsea  matumaini  huku  Napoli wakipiga  goli kupitia  Cavani  1 na  Lavezi  2.  Ujio wa  kocha mpya  Robert  Di  Mateo  uliipa nguvu  mpya clabu yachelsea  nakuifanya iizabue   magoli 4-1 Napoli pale  ilipoenda  darajani Stamford Bridge  goli za  Didier Drogba, John Terry na Frank Lampard.


AC Milan 2-0 FC Barcelona
FC Barcelona 4-0 AC Milan

2012/13 round of 16

 Hakuna timu ambayo imewahi kushinda mechi ya kwanza 2-0 alafu ikashindwa kujipatia angalau goli moja la ugenini,  lakini   Barcelona ilifanya  kweli pale ilipokub ali kipigo cha goli 2-0 pale Sansiro  na kuweza kushinda goli 4-0.

Olympiacos FC 2-0 Manchester United FC
Manchester United FC 3-0 Olympiacos FC
2013/14 round of 16

 Hamasa ya  Sir  Alex Ferguson  ilisaidia  kuwapa wachezaji wake nguvu ya ajabu pale walipo  kubali goli 2-0 dhidi ya  Olimpiacos FC na  kuweza kushinda goli 3-0, goli za  Robin Van  Persie  2  na Joel Campbell.
Kipigo hicho kiliidhoofisha Olimpiacos na kuondoa ndoto yake kwenda hatua   ya  robo fainali  kwa  mara  ya kwanza.

Paris Saint-Germain 3-1 Chelsea FC
Chelsea FC 2-0 Paris Saint-Germain
2013/14 quarter-finals

Chelsea kwa  mara nyingine tena lakini kipindi  hichi ilikua  chini ya Jose Mourinho  ni pale ngwe ya kwanza Chelsea ilipofungwa goli 3-1  goli moja lakujifunga la David Luiz na  goli la dakika ya 93  la David Luiz. Ngwe ya pili goli la penalti la  Eden Hazard na baadae  mchezaji aliye  ingia  kutokea bechi Demba  Ba alifunga goli  la ushindi lililoiwezesha Chelsea kufuzu kwa hatua  ya  robo final.

Bonus  Comeback

FC Porto 3-1 FC Bayern München
FC Bayern München 6-1 FC Porto
2014/15 quarter-finals

    TOA MAONI YAKO   KWA  KUKOMENTI  CHINI  HAPO!!
 
 Cridit&sources:  Uefa.com,  wikipedia  and  arsenal.com

No comments:

Post a Comment