Arsene Wenger amekua akijihusisha na kutaka kusajili washambuliaji wengi nguli kama vile Cristiano Ronaldo, Zlatan Ib rahimovic, Luis Suares, Gonzalo Higuain, Sergio Aguero na wengine wengi, lakini kutokana na sababu mbalimbali ambazo kocha wa Arsenal anazijua mwenyewe
10. Tomas Danilevicius
Wenger alitoa paundi ya Uingereza milioni 1 kwa mshambuliaji wa Lithuania mnamo mwaka 2000. Alicheza mara mbili kwenye ligi ya EPL lakini hakufanikiwa kufunga goli na hakuweza kucheza tena.
9. Jeremie Aliadiere
Mtoto wa Akademia ya Arsenal alicheza katika nafasi ya akiba na akicheza katika mechi za vikombe. Raia huyu wa Ufaransa aliweza kufunga goli 1 tuula ligi, hadi alipofikisha umri wa kati ya miaka ya 25 aliauzwa .
8. Andrey Arshavin
Mshambuliaji wazamani wa Arsenal na raia wa Russia. Kusema kweli Arshavin alikua katika kiwango kizuri alipokua kicheza nafasi ya mshamb uliaji wa pili lakini mashabiki wa Arsenal na Arsene Wenger mwenyewe hawezi kukubali kua thamani ya Paundi 12 milioni zilitendewa kazi na Wenger.
7. Christopher Wreh
Christopher Wreh a,baye ni binamu wa George Weah alisajiliwa na Arsenal kwa kitita cha paundi 300,000 za Uingereza akitokea Monaco. Aliifungia Arsenal goli 4 tuu baada ya hapo alipotea kabisa katika dira ya kandanda.
6. Nicklas Bendtner
Bendtner alijiunga na klabu ya Arsenal akiwa kijana mdogo na alifanya vizuri sana akitokea benchi kama mchezaji wa akiba. Akiamini kua Bendtner ameshakua mshambuliaji bora wa dunia Wenger alimpa nafasi lakini Bendtner alishindwa kuonyesha kiwango kilichotarajiwa.
5. Kaba Diawara
Diawara alisajiliwa na Wenger 1998. Alichezea klabu ya Arsenal kwa msimu mmoja tuu, alichezea mechi 15 hakufanikiwa kufunga goli hata moja (japokua aligongesha myamba mara nyingi), usajili wa paundi za Uingereza 2.5 milioni haukufanya kazi nzuri.
4. Gervinho
Gervinho alisajiliwa kwa kitita cha thamani ya paundi milioni 10 ya Uingereza. Japokua alikua akipiga sana vyenga vya maudhi alikua akikosa nafasi kadha wa kadha na kumfanya ajihisi ni mwenye hatia na alikua kero kwa mashabiki wake.Alicheza mechi 45 na kufunga goli 9 tuu.
3. Park Chu Young
Moja kati ya usajili mbovu kabisa wa Arsene Wenger alipo amua kumsajili mchezaji huyo rai wa Korea lengo ili aweze kuuza jezi za Arsenal huko Mashariki ya mbali. Park Chu Young hakuweza kufanya lolote lile na kuamua kumpeleka kwa mkopo nchini Spain klabuni Celta Vigo.
2. Marouane Chamakh
Wenger alimsajili Marouane Chamakh kutoka Bordeaux kwa usajili huru lakini kamali ya usajili haikuweza kuzaa matunda. Mshambuliaji huyo wa Moroco aliweza kuifungia Arsenal goli 8 tuu katika mechi 40 alizochezea klabuni hapo.
1. Francis Jeffers
Alisajiliwa kutokea klabu ya Everton kwa kitita cha paundi milioni 8, alifanikiwa kufunga goli 4 tuu katika kipindi cha miaka 3 aliyowezakuchezea pale arsenal. Japokua hakuonekana kama ni mchazaji muhimu w a Atsenal alifanikiwa kujinyakulia vikombe viwili vya FA na ligi kuu ya Uingereza 1.
Author: Livingdream
Sources: English Premier League, arsenal.com
wenger bonge la fara yani anashindwa kusajiri strikers bora anakalia kusajili magarasa tuu!!
ReplyDeleteAnasema haondoki hata msimu ujao atakuwepo 2018
ReplyDelete