Saturday 4 March 2017

Washambuliaji 10 Wabovu Kabisa Wa Arsene Wenger

By:  LivingDreamer

Arsene Wenger  amekua  akijihusisha na kutaka kusajili washambuliaji wengi nguli kama vile Cristiano  Ronaldo,  Zlatan Ib rahimovic, Luis  Suares,  Gonzalo  Higuain,  Sergio  Aguero  na wengine wengi, lakini kutokana na sababu mbalimbali  ambazo  kocha wa Arsenal anazijua mwenyewe



10. Tomas Danilevicius
 Wenger  alitoa  paundi ya Uingereza  milioni  1   kwa mshambuliaji  wa  Lithuania mnamo mwaka 2000.  Alicheza mara mbili  kwenye  ligi ya EPL  lakini hakufanikiwa  kufunga goli  na  hakuweza kucheza tena.

9. Jeremie Aliadiere
Mtoto  wa  Akademia ya  Arsenal  alicheza  katika  nafasi ya akiba na  akicheza katika mechi za vikombe.  Raia huyu wa Ufaransa  aliweza  kufunga  goli  1 tuula ligi,  hadi  alipofikisha  umri wa  kati ya  miaka  ya 25 aliauzwa . 

8. Andrey Arshavin
Mshambuliaji wazamani wa Arsenal  na  raia wa RussiaKusema kweli  Arshavin  alikua katika kiwango kizuri alipokua  kicheza nafasi  ya mshamb uliaji  wa pili lakini  mashabiki wa Arsenal  na Arsene Wenger  mwenyewe hawezi kukubali kua  thamani ya Paundi 12 milioni zilitendewa  kazi  na Wenger.
 
7. Christopher Wreh
Christopher  Wreh  a,baye  ni  binamu  wa  George  Weah  alisajiliwa  na Arsenal kwa kitita cha paundi 300,000 za Uingereza  akitokea Monaco.  Aliifungia  Arsenal  goli 4  tuu baada ya  hapo alipotea  kabisa  katika dira ya kandanda.    

6. Nicklas Bendtner
Bendtner alijiunga na  klabu ya Arsenal akiwa kijana mdogo  na alifanya vizuri sana akitokea  benchi kama mchezaji wa akiba.  Akiamini kua  Bendtner  ameshakua  mshambuliaji bora  wa dunia  Wenger alimpa  nafasi lakini  Bendtner alishindwa kuonyesha kiwango  kilichotarajiwa.  

5. Kaba Diawara
Diawara  alisajiliwa  na  Wenger  1998.  Alichezea klabu ya  Arsenal kwa  msimu  mmoja  tuu,  alichezea  mechi  15  hakufanikiwa kufunga goli  hata  moja (japokua aligongesha myamba  mara nyingi),    usajili wa paundi za Uingereza 2.5  milioni haukufanya  kazi nzuri.

4. Gervinho
Gervinho alisajiliwa kwa  kitita  cha thamani ya paundi milioni 10 ya Uingereza. Japokua alikua akipiga sana vyenga vya maudhi alikua akikosa  nafasi kadha wa kadha  na  kumfanya ajihisi  ni  mwenye hatia na alikua kero kwa mashabiki wake.Alicheza  mechi  45  na kufunga goli 9 tuu.

 3. Park Chu Young

Moja kati ya usajili mbovu kabisa wa Arsene Wenger  alipo amua kumsajili mchezaji  huyo rai wa  Korea lengo ili aweze kuuza jezi za Arsenal huko  Mashariki ya mbali.  Park Chu Young hakuweza kufanya lolote lile na kuamua kumpeleka kwa mkopo nchini  Spain klabuni Celta  Vigo. 

2. Marouane Chamakh
Wenger alimsajili Marouane Chamakh  kutoka Bordeaux  kwa usajili huru  lakini kamali ya usajili haikuweza  kuzaa  matunda. Mshambuliaji huyo wa Moroco aliweza kuifungia Arsenal  goli 8 tuu katika mechi 40 alizochezea klabuni hapo.

1. Francis Jeffers
Alisajiliwa kutokea klabu ya Everton  kwa  kitita cha paundi  milioni 8,  alifanikiwa kufunga goli 4 tuu katika kipindi cha  miaka  3 aliyowezakuchezea pale arsenal.  Japokua   hakuonekana kama ni mchazaji  muhimu w a Atsenal alifanikiwa kujinyakulia vikombe viwili vya FA  na ligi  kuu ya Uingereza  1.

Author: Livingdream
Sources: English Premier League,  arsenal.com
 

2 comments:

  1. wenger bonge la fara yani anashindwa kusajiri strikers bora anakalia kusajili magarasa tuu!!

    ReplyDelete
  2. Anasema haondoki hata msimu ujao atakuwepo 2018

    ReplyDelete