Thursday 20 April 2017

Zijue Hofu 10 Zinazo Mfanya Binadamu Ashindwe Kufanikiwa Kimaisha

Mwandishi: Living Dreamer


Hofu inauwezo mkubwa sana wa kukurudisha nyuma katika kazi, uhusiano, na kushindwa kufanikisha ndoto zako. Angalia kwa undani kabisa hofu kumi ambazo ni changamoto kubwa na ufanye unyambuzi yakinifu juu ya hofu zipi/ipi ambazo zinakusumbua na jinsi gani uweze kuepukana nazo.

#1. Hofu Ya Kukataliwa
Watu wengi huogopa kuingia katika mahusiano mapya au kukutana na watu wapya kwa hofu ya kukataliwa. Hata kwa wanandoa ambao wapo katika uhusiano wa muda mrefu huofia kupendekeza jambo jipya kwa kuhofia kukataliwa na mwenza wake. Pia hofu ya kuogopa kumuomba bosi wako akuongezee mshahara kwa hofu ya kukataliwa, au mtu mwenye mvuto kua hataweza kukubali kuwa katika mahusiano na wewe kwa sababu ambazo huna uhakika nazo. 

Jinsi ya Kuondoa Hofu Hii
Usihofie kukataliwa katika jambo lolote, kukataliwa ni sehemu tu ya maisha, hakuna mtu atakaye pendwa na watu wote. Kukataliwa ni sehemu moja wapo ya hamasa ambayo binadamu akiitumia anaweza kupata mafanikio ya ajabu, Mfano: Mfanyakazi anapoenda kumuomba bosi wake amuongezee mshara kwa kile anachokiamini kazi anayoifanya ni kubwa zaidi kuliko kipato anacho kiingiza mwisho wa kila mwezi, lakini bosi anavyoipata taaarifa hiyo anakataa kumuongezea mshahara. Kuna mitazamo ya aina mbili 1. Mtu anaweza kujiona anamkosi na akakata tamaa kabisa ya maisha na 2. Mtu mwingine anaweza kuichukua nafasi hiyo kwa kutafuta njia nyingine ya kuweza kujipatia kipato kizuri zaidi kama vile kutafuta kazi sehemu nyingine yenye maslahi mazuri zaidi au kuanzisha biashara zake mwenyewe.


#2. Hofu Ya Kushindwa
Kati ya hofu kubwa kabisa duniani ni hofu ya kushindwa. Watu wengi hua hawataki kujaaribu kitu chochote kipya hadi wajilidhishe kua ni lazima watafanikiwa. 

Jinsi ya Kuondoa Hofu Hii  
Kushindwa ni sehemu ya maisha ya kawaida ya binadamu na kujifunza kutokana na makosa hua ndio njia sahihi ya kufanikiwa kimaisha. Watu wengi walio fanikiwa kimaisha siku zote husema ni mara nyingi walishindwa katika kazi au biashara fulani lakini walinyanyuka tena na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa. Usikate tamaa ukishindwa katika jambo lolote rudia hata ikibidi mara 1000 hadi ufanikishe ndoto yako, watu waliofanikiwa hua hawakati tamaa.


#3. Hofu Ya Kutokua Na Uhakika
Kwa kawaida hofu ya kutokua na uhakika huwafanya watu washindwe kufanya vitu vingine vipya. Kwa kawaida hua na woga, kwa mfano "Itakuaje kama sitokipenda hicho kitu kipya" au "watu watanionaje au watasemaje juu ya hichi kitu kipya" hofu hii huwafanya watu washindwe kufanya vitu vipya na huendelea kufanya vitu kwa njia ileile hata kama havina manufaa yoyote katika maisha yao.
Jinsi ya Kuondoa Hofu hii
 Mtu maarufu zaidi katika karne ya 20 bwana Albert Enstain alisema "Insanity is doing the same thing over and over again and expecting different results " akimaanisha ni uwendawazimu kufanya jambo lile lile kwa njia zilezile na kutegemea kupata matokeo tofauti. Basi ni vyema tujifunze kutoka kwa watu waliofanikiwa katika maisha, hufanya mambo mengi tofauti ili kufanikisha ndoto zao za kuwa na mafanikio. 
#4. Hofu Ya Upweke
Muda mwingine watu hukaa katika mahusano yasiyokua na maelewano au hougopa kuishi peke yao kwa kuhofia kua wapweke.
Jinsi ya Kuondokana na hofu hii
Jifunze jinsi ya kuvumilia upweke kwa muda huku muda huo huo ukijifunza njia itakayokufanya uweze kuondokana na upweke unaokusumbua. Mfano unaweza ukajikita katika ibada au maombi, kushiriki katika semina mbalimbali, michezo, kusoma vitabu au kutafuta rafiki ambaye mtakua nayekaribu ambaye mtakua na uwezo wa kushirikishana changamoto na jinsi gani ya kuzitatua hizo changamoto.


#5. Hofu Ya Kufanya Mabadiliko
Tunaishi katika dunia ya mabadiliko ya haraka sana. Lakini katika hali ya kushangaza watu bado huogopa kufanya mabadiliko. Hofu ya kufanya mabadiliko huwafanya watu wadumae kifikra na kushindwa kutumia fursa zinazojitokeza katika mabadiliko ya kimaisha.
Jinsi ya Kuondoa hofu Hii
Wakati mwingine inabidi kufumba macho na kuamua kufanya mabadiliko japo kidogo kamavile hatua za mtoto mdogo. Mfano mtu umeajiriwa na unalipwa mshara mdogo ambao haunamaslahi yoyote kwa maisha yako ya sasa na baadae, ni vyema kutafuta njia sahihi itakayo weza kukupatia kipato cha kutosha kwa kujifunza wengine wanafanya nini(kusoma maisha ya watu waliofanikiwa na mbinu walizozitumia) na ikiwezekana uweze kuanzisha miradi midogo midogo ukiwa na ndoto ya kuja kuwa na mafanikio katika biashara kubwa.

#6. Hofu Ya Kukosa Uhuru
Hofu hii ni kati ya hofu ambayo huwafanya watu washindwe kufanya maamuzi mengine kwa kuhofia uhuru walionao unaweza kupotea. Mfano watumishi wengi wa serekalini wamekua wakiishi katika hali ngumu sana kimaisha lakini siku zote utawasikia wakisema wanafurahia uhuru wa kazi wanaopewa na mwajiri wao mkubwa ambaye ni serikali. Hapa utaona mshara wa mwalimu ni mdogo ambao hauna uwezo wa kumfanya ajenge nyumba au awezekufanya maendeleo makubwa kwa ajili yake na familia yake.
Jinsi ya kuondoa Hofu hii
Kuna uhuru wa kweli na uhuru wa kutokujiamini, tuangalie katika mfano wa mwajiriwa wa serekalini amabye anaamini anauhuru katika ajira yake huku kipato anachokipata kinazidiwa na Mangi Muuza duka kila mwisho wa mwezi. Kuna kitu wataalamu tunaita Financial freedom na Job freedom. Job freedom ni uhuru wa kazi ambao hauna maslahi ya kiuchumi katika maisha ya mwajiriwa moja kwa moja, na financial freedom uhuru wa kiuchumi ambao hua haupatikani kwa mtu kua mwajiriwa bali mtu kujiajili na kuweza kumiliki biashara zake mwenyewe.

#7. Hofu Ya Kuhukumiwa
Watu ambao huofia kuhukumiwa na watu wengine siku zote hushindwa kufanya maamuzi yoyote yale hasa ya kijamii kwa kuhofia watu watamuhukumu vibaya pale atakapo kosea.  Watu ambao wameshikwa na hofu ya aina hii  muda mwingi utawasikia wakilalamika na kuzungumzia kwa ubaya tuu jinsi gani watu watawasema vibaya endapo wakikosea.
Namna ya Kuondokana na Hofu hii
Jaaribu kuelewa kuwa kila mtu anamaoni yake juu ya kitu fulani katika maisha, hata uwe mwema kiasi gani wapo watakao kupenda na wapo watakao kuchukia. Jifunze kupenda kile unachokifanya kwa maana ndoto hukamilishwa na mwota ndoto mwenyewe hivyo basi maoni ya watu wengine isiwe sababu ya wewe kushindwa kufanikisha ndoto zako za kimaisha.

#8. Hofu Ya Kutokewa Na Jambo Baya
Mambo mabaya hutokea katika maisha, ni kitu kisicho epukika. Hivyo basi watu wengine hua ni waoga kupindukia muda wote na kupelekea kushindwa kufanya mambo mengine katika maisha. Mfano kunamchezaji nguli wa zamani wa soka wa Arsenal Denis Bergkamp alishagoma kabisa kupanda ndege kwa hofu ya kupata ajali. Kunahofu nyingi huu ni mfano mmoja tuu lakini watu wengine wanaogopa usiku wakiamini majini au wachawi watakuja kuwawangia, watu wa namna hii wanashindwa kulala vyema hivyo kupelekea ufanisi wao katika kazi kupungua au kushindwa kabisa.

Namna ya kuondoa Hofu Hii
Uoga si kitu cha kweli, unaweza kuatengeza au kuuondoa. Hivyo basi kunanjia  nyingi za kuondoa hofu ya aina hii kama vile kujikita zaidi katika sala, kulala muda mrefu, kusoma vitabu vya ujasiri wa watu wengine au kuhudhuria matibabu ya washauli wa kisaikolojia.

#9. Hofu Ya Kuumizwa
Watu wengine hushindwa kutimiza ndoto zao katika maisha kwa kuhofia wanaweza kuumia. Mfano nilipokua mdogo nilikua mpenzi sana wa mchezaji mpira Ronaldo Luiz Nazario De Lima na nilikua nikiamini ipo siku moja nitakuja kua kama yeye, lakini baba yangu alikua akiniambia nitavunjika mguu na kushindwa kuendelea na masomo hii iliniingia akilini na kuamini ipo siku moja nitavunjika hivyo ndoto yangu ikayeyuka kama barafu jangwani. Hofu hii hufanya watu wengi kushindwa kutimiza ndoto na malengo yao katika maisha.

Namna ya Kuondoa Hofu Hii
Dunia imejaa maumivu mengi huna uwezo wa kuepuka maumivu, hata kama utajifungia ndani ya kabati la nguo maumivu yatakufuata hapo hapo ulipo. Njia sahihi ni kutakiwa kuelewa katika mafanikio yoyote yale kuna sehemu ya maumivu yake. Hakuna mtu aliyefanikiwa katika maisha bila ya kupata maumivu.

#10. Hofu Ya Kutokua Na Elimu
Aina hii ya hofu huwakumba watu wengi , kuhofia hawana uwezo wa kutosha wa kufanya jambo fulani. Watu wengi huogopa kuchukua nafasi ya mafanikio kwa kuhofia hawapo vizuri kielimu hii huwafanya kushindwa kufanya kazi wanazopewa au nafasi za kazi wanazopata.
Namna ya Kuondoa Hofu Hii
Amini usiamini elimu pekee yake sio kipimo cha kujua vitu au uwezo wa kufanya vitu, hivyo basi unapopata nafasi ya kufanya kazi usiache kwani taaluma ya ufanyaji kazi ni tofauti na taaluma ya vitabuni. Bill Gates hana Degree lakini ndiye mtu tajiri zaidi duniani, sasa unaweza ukajiuliza kuna maprofesa na madaktari wangapi duniani lakini kwanini hawana mafanikio ya mtu ambaye hana elimu kama wao?
'Big Dream Attracts Big People and If You can Dream then You can Do it'
Evarist Isdory


TOA MAONI YAKO NI HOFU GANI ULIYO 
UNAFANYAJE KUIONDOA HOFU YAKO


SHARE TO YOUR LOVERS 

1 comment:

  1. Ignition will then ask you for some info, together with your full name and cellular quantity. Withdrawals most likely to|are inclined to} take now not than 2 days regardless of your banking technique, and reside chat is on the market. Overall RTP for all games, meanwhile, is an impressive ninety eight.32%. Launched in 2016, Cafe Casino has always been out there as 카지노사이트 a cellular web site. This has allowed the staff behind it to fine-tune its providing, so that today’s cellular experience is seamless, fast, and intuitive.

    ReplyDelete