Friday 14 July 2017

Siri 10 Za Mafanikio ya Nick Cannon

Writter: SirGwaje


Evarist G.I : Siri ninayo ipenda zaidi kutoka kwa Nick ni siri #1 kuwa chemchem ya hamasa yako.Usisubiri watu wengine waseme unaweza, anza kuwezandani ya nafsi yako mwenyewe.

"Jitahidi uwe katika ubora wako kwa jitihada zako zote
"Maisha yangu ni ushuhuda tosha, kuyapa maneno yanayozungumzwa uhai. Kama unavyojua ninaishi ndoto zangu" 
"Malengo ni mfalme, Malengo siku zote yatazidi kushinda"

Siri 10 Za Nick Cannon
1. Kua chemchem ya hamasa yako
2. Jiamini
3. Kuwa mkweli
4. Jifunze kutoka kwa wengine
5. Fanya wewe mwenyewe
6. Kuwa na mtazamo
7. Simamia ndoto yako
8. Fanya kwa njia yako
9. Kuwa dereva
10. Kuwa mwenye furaha 

Nick Cannon - Siri 10 za Mafanikio

Siri#1: Kua chemchem ya hamasa yako
Kila siku hua ninasema mtu anatakiwa awe ni chemchem ya hamasa yake. Unapo amka na kutoka nje kila siku unakutana na watu wanao kukatisha tamaa, wanao kuchukia, na wale wanaosema maneno mengi lakini wao wenyewe hawafanyi kitu chochote na wale wengine wanaosema hutaweza kamwe kufanikiwa katika jambo lolote lile. Njia pekee ni kusema ndani ya nafsi yako kua jambo hili ninalo lifanya lina maana sana na kuamini kua ni lazima tuu litafanikiwa. Sema kila siku hili jambo ninalolifanya ni lazima litafanikiwa na pia unatakiwa uamini kwa vitendo.


Siri#2: Jiamini
Jitahidi uwe katika ubora wako kwa judhudi zako zote. Jitolee kwa kile unachoweza kujitolea kila siku. Watu wengi hua wanafanya kosa kubwa kwa kua na kiburi zaidi. Kitu cha msingi tunacho kizungumzia hapa ni  kujiamini kwa kuwa na mtazamo wa mbele. Kaa ndani ya chumba chako, tembea kila kona ukitafakari ni jinsi gani unao uwezo wa kufanya mambo makubwa katika dunia hii.

 
Siri#3: Kua mkweli
Hakika unapaswa kuwa mkali, na mwelevu, na mtaalamu wakati wote wakati ukionyesha maoni yako, na kuna muda na mahali pa kusema mambo fulani.Na unajua, wakati mwingine washirika fulani hawawezi kukubaliana na kile ninachosema. 

Mhojaji: Je! Umewahi kufanya jambo hilo? 
Nick: Ooh!! Wakati wote. Lakini unajua nini? Mwisho wa siku, nawaambia watu mara nyingi hii, mimi sio mfano mzuri tu wakuigwa. Mimi ni mfano halisi.Mfano wa kuigwa ni nafasi ambayo kila mtu anauwezo wa kuelekezwa na akaweza kucheza nafasi hiyo. Ikiwa unataka, utajua, tabia ambayo unaweza kuona hapa. Lakini jambo hapa ni uhalisia katika kila aina, watu wengi hupenda kufanya kazi na watu ambao wapo na uhalisia wao na pia mtu awe mkweli.

Kua halisi na mkweli. 

 
Siri#4: Jifunze kutoka kwa wengine

 Kuna watu wengi wenye busara katika jamii yetu bado wapo hai na ninahisi kama watu hawatumii faida  ndani ya rasilimali hizo za watu kama Harry Belafonte, Sydney Poitier, na Quincy Jones. Watu wa aina hiyo ni watu ambao bado wapo na wamefanya mambo makubwa.
  
 WatuWalio jitengenezea njia  na waliojikusanyia taarifa nyingi sana, ujuzi na maarifa. Wanakila kitu, hivyo basi hatuna budi kuwafuata, kuwasoma na kuchukua utaalamu kutoka kwao na kuja kufanya kama wao wanavyofanya.

Siri#5: Fanya wewe mwenyewe
Ni kuhusu kizazi cha kibinafsi, unapaswa kuwa kukiendeleza kizazi binafsi. Sio muda wa kumsubiri mtu yoyote yule. Moja ya sababu kwa nini Corey Gunz ni mojawapo ya MCs mkali katika mitaa ni kwa sababu alifanya hivyo mwenyewe. Yeye hakungoja lebo ya rekodi, hakumngojea mtu aingie na kusema nitakupeleka hapa. Alifanya hivyo tu.Alitoka huko, na hayo ndiyo mawazo ya vijana leo. Ni muda wa kufanya kweli sasa hivi usingoje kesho.



Siri#6: Kuwa na mtazamo
Ninapenda kuwapa watu motisha, na naamini, unajua, maisha yangu ni ushuhuda tosha ninafanya maneno yanayozungumzwa yawe ya kweli.Unatakiwa kujua kuishi ndoto, na unatakiwa  kutambua nini unataka katika maisha na itakua na maana kubwa sana kwako. Hivyo basi nadhani umejua mimi ni mtu mwenye mtazamo wa mbali na ninaheshimu ndoto zangu.

Siri#7: Simamia ndoto yako
Najua inaweza kuwa na shida mara kwa mara. Nawahakikishia ninyi watu tayari mmegundua jinsi gani ilivyo ngumu kusimamia ndoto zako. Na inaweza kuwa ngumu juu ya ndoto hizo, vitu ambavyo huona  kweli kama  unataka kuvikamilisha, lakini mambo yanakwenda ndivyo sivyo. Ninawaomba siku zote msimamie ndoto zenu, msikate tamaa. Mtaweza kusimamia ndoto zenu kwa nguvu zenu zote?





Siri#8: Fanya  kwa njia yako
Jambo lililo gumu muda mwingine ni kufikiri jinsi gani watu watapokea kazi zetu. Na wakati mwingine inaweza kuwa mapambano ya ndani, lakini tena, maudhui ni mfalme. Maudhui yatashinda daima, kwa hiyo ni kuhusu kile unachofanya na jinsi unavyofanya, na taarifa ambayo inafanya.

 
Siri#9: Kuwa dereva
Unatakiwa utoke nje na ufanye na utengeneze vitu ambavyo havipo. Kama unataka hicho kitu basi huna budi kua, kuishi, kutembea na kutengeneza hicho kitu. Je, unafikiri hii inaweza ikawa ni njia moja wapo ya mafanikio?  Unachotakiwa ukifanye ni kuchukua wazo lako na kuifanya liwe tunda.




Siri#10: Kuwa mwenye furaha 
Jitahidi uwe mtu mwenye furaha katika kila jambo ambalo unalifanya, iwe kazini, michezoni, katika familia, unapokua na marafiki nk. Furaha ni sehemu muhimu sana kwenye maisha ya mwanadamu. Siku zote watu hua wananishangaa ni kwanini hua ninaoneka kama mwendawazimu ninapokua jukwaani, ukweli ni kwamba bila kuwa na furaha hutoweza kamwe kudumu katika kazi unayo ifanya na kupelekea usiwe na mafanikio stahiki.



Nick Cannon Quote
"
I was 16 years old, driving to LA, and sleeping in my car, just trying to make it happen."



SHARE IT!!!
COMMENT BELOW TO INSPIRE OTHERS
MAKE THE WORLD SUCCESS  AGAIN
Remember: Success Doesn't Follow a Time Clock

Credit: Evan C., TheActiveDreamer, Words of wisdom.

1 comment:

  1. Play Roulette Online | Best Roulette Sites & Casino Sites for Real
    Discover the best online casino 188bet for 온라인카지노 Roulette matchpoint games, where to play the game, strategies, free spins, roulette, craps, roulette and more.

    ReplyDelete