Je, wapenzi na mashabiki wa Ligi ya ndani ya Vodacom Premier League ya Tanzania bado wana mapenzi ya dhati dhidi ya ligi yao? Je, ni mashabiki wangapi ambao wataenda katika vituo mbalimbali vya kuonyeshea mpira wa EPL katika muda sawa ambao ligi kuu ya VPL inachezwa?
Mashabiki na wapenzi wa soka nchini Tanzania wanao uwezo wa kutaja vikosi vya timu za ulaya hasa EPL, Serie A na La Liga, lakini jaaribu uwaulize kuhusu timu zao za ndani asilimia kubwa ni lazima watashindwa tuu, nawatakao jitahidi wataishia kutaja majina ya wachezaji wawili au watano bila kujua umri wa wachezaji wao wala mikataba yao na wapi wanapotokea.
Wamiliki wa
vilabu, shirikisho la soka na wizara ya michezo nchini
wanafahamu hawana maslahi na shauku ya ligi ya ndani, kutokana na umaarufu wa Ligi Kuu ya England, La Liga, Bundesliga, Serie A na France
Ligue 1.
Ustadi wa ligi kuu ya Tanzania Bara EPL unarudishwa nyuma na mashabiki wa jadi ambao huamini kuangalia mpira wa ndani ni sawa na kupoteza muda wao bure, au kuvaa jezi ya timu ya ndani ni sawa na kujidhalilisha. Hii inapelekea mapato ya timu kupungua kila kukicha sababu watu hawanunui jezi za timu zao na kujikuta wakivaa jezi za timu kama Arsenal, Barcelona nk.
5. Maudhurio Mabovu ya Mashabiki
Wakati wa siku
za mechi, wapenzi wa soka hukusanyika kwenye baa za nguvu ili
kuangalia michezo ya timu zao za Ulaya wanazozipenda kwenye skrini kubwa, na kusahau debi inayochezwa kwenye uwanja wa karibu. Badala
yake hutumia kiasi cha shilingi 1000-15000, huwekeza
muda kwa kuangalia Arsenal au Chelsea wakati wanakunywa bia baridi na marafiki hua
inaonekana kuwa bora zaidi.
Vilabu huendelea kuandikisha idadi ndogo ya mashabiki kila siku za mechi, isipotokea kuna timu kubwa au finali basi idadi hua ni ndogo sanahivyo kufanya mapato ya siku kuwa madogo na yasiyo ridhisha. Mechi za mikoani idadi hua kubwa tuu pale ambapo timu za Simba na Yanga zinapokwenda kucheza.
4. Haki za Maonyesho ya Television
Ligi ya Tanzania inaendelea kupoteza udhamini mkubwa wa maonyesho ya televisheni kutokana na idadi ya watazamaji kupungua sana. Baadhi ya wamiliki wamekua wakishindwa kuongeza mikataba ya kuonyesha soka kwenye luninga kwa sababu ya ukosefu au idadi ndogo ya watazamaji amabo hupelekea kutopata wadhamini wasaidizi wa kuweza kurusha vipindi vya mpira moja kwa moja.
Sio kwa Tanzania peke yake lakini nchi nyingi za ukanda wa Afrika zimekua zikishindwa kurusha vipindi mpira wa miguu live kutokana na kukosekana kwa wadhamini.
3. Kutokuwa Tayri Kukaa Kwenye Ligi
Wachezaji wengi kama sio wote wa Tanzania hua wanacheza mpira lakini akili yao hua nje ya nchi kama vile ulaya, Afrika Kusini, Arabia na China ambayo imekuja kwa kasi sana hivi sasa.
"Ni nani anayefurahia kucheza hapa, sisi sote tunataka kwenda Ulaya na kucheza mpira wa miguu bora katika hali nzuri, na kuachana na hali hii kwa mapenzi ya Mungu,"
Maneno yaliyosemwa na mchezaji mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe.
"Tunajitayarisha na kuja kucheza ili tuheshimu ratiba zetu bila kutarajia mengi kutoka kwa mashabiki kwa sababu hawaji tena kwenye viwanja. Timu zetu na ligi haiwezi kuboreka katika hali hii. Inafanya maisha yawe magumu kwa kila klabu ya Afrika, "
Hamasa ya wachezaji wa ndani kua mbovu, na maudhurio mabaya ya mashabiki inafanya ligi yetu pendwa ya VPL izidi kuwa dhohofuli hali.Djibril Drame, coach of Mali champions Stade Malien
2. Uwekezaji Duni
Wafanya biashara wakubwa hawataki kumiliki timu za mpira wa miguu za Afrika kama wanavyotaka kumiliki timu za Ulaya, Amerika na Asia kutokana na sababu ya kutokuwepo hamasa ndani ya nchi husika na kuto kuvutia kipesa.
Vilabu vingi vinashindwa kupata mikopo katika mabenki, kutokana na kutokuwepo kwa uhakika wa kurudisha mikopo. Vilabu vingi vimekua vinategemea kupata ruzuku kutoka serekalini kama sehemu yao kubwa ya kujiendesha, lakini ukweli ni kwamba ruzuku haina uwezo wa kutosheleza mahitaji yote ya timu ikiwa ni pamoja.
1. Uchaguzi wa Kazi (Proffesional Career)
Inaonekana kuwa ni kesi katika nchi nyingi za bara kwamba wachezaji wa Afrika ambao wanafanikiwa kucheza ligi za nje ya nchi hua wanakua na heshima na maarufu zaidi, jambo ambalo linatoa nafasi ya upendeleo kwa FA na wapenzi wa soka kwa ujumla. Wachezaji wanaocheza nje za nchi kama Mbwana Samata wamekua na uwezo mkubwa wa kipesa tofauti na wachezaji wa ndani , hivyo kupelekea kila mchezaji wa ndani awe anafikiria kwenda kucheza Ulaya tuu.
THANKS FOR VISITING US!
SHARE TO YOUR FRIENDS
&
COMMENT HAPO CHINI..
There are no secrets to success. It is the result of preparation, hard work, and learning from failure.
Colin Powell
Read more at: https://www.brainyquote.com/quotes/quotes/c/colinpowel121363.html?src=t_business
Read more at: https://www.brainyquote.com/quotes/quotes/c/colinpowel121363.html?src=t_business
There are no secrets to success. It is the result of preparation, hard work, and learning from failure.
Colin Powell
Read more at: https://www.brainyquote.com/quotes/quotes/c/colinpowel121363.html?src=t_business
Read more at: https://www.brainyquote.com/quotes/quotes/c/colinpowel121363.html?src=t_business
"Lazima uheshimu watu, na lazima uheshimu fedha. Baba yangu aliniambia: 'Unapoheshimu pesa, fedha zitakuheshimu.'
Yaya Toure"
There are no secrets to success. It is the result of preparation, hard work, and learning from failure.
Colin Powell
Read more at: https://www.brainyquote.com/quotes/quotes/c/colinpowel121363.html?src=t_business
Read more at: https://www.brainyquote.com/quotes/quotes/c/colinpowel121363.html?src=t_business
WASASILIANA NASI KUPITIA
Mob No: 0171411775 / 0753033101 / 0715411245
Barua Pepe: isdorykitunda@gmail.com/sirgwaje@gmail.com
No comments:
Post a Comment