Kama upo makini na unataka kuwa mtu mwenye mafanikio katika maisha yako basi huwezi kufanya kitu kingine kizuri zaidi ya kujielimisha mwenyewe kwa kujifunza na kuwasoma watu waliofanikiwa na maarufu.
Watu wengi wanaotaka kufanikiwa kataika maisha, kazi au biashara hushindwa kufanya hivyo kwa sababu hawajui maana ya kuwa na mafinikio au hawajui njia ya kufikia mafanikio ipo vipi. Wao huona matokeo yamwisho ambayo ni mtu mwenye mafanikio, bila kuwa na wazo lolote lile juu ya njia alizo pitia kufikia mafanikio hayo.
Kwa kujua hadithi za watu wenye mafanikio utajifunza jinsi barabara ya mafanikio inavyoonekana na nafasi yako ya kufanikiwa katika maisha itakuwa ya juu sana.
Chini ni hadithi fupi na za haraka za msukumo wa baadhi ya watu waliofanikiwa zaidi ambao wanaweza kukusaidia kujua mengi kuhusu mbinu inayotakiwa kufikia mafanikio.
- Hadithi ya Mafanikio ya Soichiro Honda: Soichiro Honda ni mwanzilishi wa kampuni ya Honda ambayo ni mojawapo ya kampuni kubwa za magari ya magari maalumu. Historia ya Honda ilianza pale alipoenda kufanya mahojiano ya kazi katika kampuni la Toyota. Honda alikataliwa na aliambiwa kuwa haifai na hana vigezo vya kufanya kazi! Mtu huyo hakuacha na akaamua kuunda kampuni inayopigana na Toyota na hivyo honda alizaliwa !! Ikiwa kuna kitu chochote tunaweza kujifunza kutokana na hadithi hii ya mafanikio ni kamwe tusikate tamaa.
- Hadithi ya mafanikio ya Stephen King: Watu wengi wanajua Stephen King kama mwandishi maarufu lakini wachache tuu wanajua hadithi ya maisha yake. Riwaya ya kwanza ya Stephen ilikataliwa karibu kila mahali kwa kiwango ambacho yeye mwenyewe akaamua kuitupa katika taka! Mkewe aliipata
hadithi kutoka kwenye takataka na kusisitiza kwamba mmewe aipeleke tena riwaya yake na hatimaye akawa Stephen King tunayemjua sasa! Kuna somo muhimu sana muhimu sana ambalo tunajifunza kutoka katika hadithi hii ya mafanikio ambayo ni hata ukataliwe vipi na watu unatakiwa uone kama haina maana yoyote ile endapo tuu unajiamini kwa kile ulichokifanya.
- Hadithi ya Mafanikio ya Thomas Edison: Hadithi ya mafanikio ya Thomas ni moja ya hadithi zinazoweza kuhamasisha mtu yoyote baada yamajaribio mengi ya kushindwa.
Thomas alishindwa mara 999 kutengeneza taa kabla ya kufanikiwa kufanya hivyo kwenye jaribio la 1000. Watu walipomwuliza jinsi ulivyoweza kuendeleza hata ingawa wewe ulikuwa unashindwa wakati wote aliwaambia kwamba, kila wakati jaribio lilivyoshindwa nilikuwa nikisema kuwa nimegundua njia mpya ya kutengeneza taa. Hadithi ya mafanikio ya Thomas Edison inapaswa kukufanya uhitimishe kuwa kushindwa isiwe sababu ya kukufanya usisonge mbele hata ikiwa ilitokea zaidi ya mara moja.
- Hadithi ya mafanikio ya Oprah Winfrey: Moja ya hadithi za za kuvutia zilizowahi kunitia hamasa nilipo zisoma kwa mara ya kwanza ni hadithi ya mafanikio ya Oprah Winfrey. Oprah
ni mojawapo ya icons maarufu zaidi ya maonyesho ya televisheni ya ana kwa ana leo na pia ni mmoja wa
wanawake matajiri duniani lakini hii sio historia ya hadithi yake
ilivyoanza. Je, unajua kwamba Oprah alifukuzwa kazi na akaambiwa kuwa hakuwa sahihi kwa TV mapema katika maisha yake? Oprah hakukata tamaa alijiamini na kuendelea kufanya mazoezi mengi zaidi hadi mwisho wa siku kuja kuwa mtu maarufu katika historia ya televisheni. Somo katika hadithi fupi ya Oprah ni kuwa mafanikio hayachagui rangi, jinsia au hata umri.
- Hadithi ya mafanikio ya Bill Gates: Bill Gates mwanzilishi wa kampuni la Microsoft alifeli masomo yake alipokua chuoni Harvard hivyo aliondolewa chuoni. Wengi wetu tungewezakutafuta nafasi katika vyuo vingine lakini sio kwa Bill Gates, yeye baada ya kufukuzwa chuoni alikuwa na mtazamo mkubwa wa kufungua kampuni yeye na rafiki yake Allen lililojulikana kama Traf-O-Data na baadae Bill Gates aliweza kuanzisha kampuni liitwalo Microsoft ambalo lilikuja kuwa kampuni tajiri na maarufu duniani. Mengine yanayobaki ni kuwa Bill Gates ndiye mtu tajiri zaidi duniani. Somo katika historia hii fupi ya Bill Gates ni elimu ya darasani pekee sio njia ya kukufanya uwe na mafanikio.
- Hadithi ya mafanikio yangu binafsi: Mimi sina mafanikio kama hao waliotajwa hapo juu, lakini nipo katika njia sahihi ya kufanikiwa kama wao. Baada ya kumaliza chuo kikuu nilikaa mtaani kwa takribani miaka mitatu bila ya kupata ajira baada ya muda nilitumia video moja ya animation iliyokua inaelezea kitabu maarufu cha Rich Dad Poor Dad kutoka siku ile nilianza kusoma vitabu vya watu waliofanikiwa na ndio nikaja na wazo la kufungua Blogu , Yooutube channel na nipo katika mchakato wa kufungua kampuni linalohusu maswala ya teknolojia ya mawasiliano na ninaandika kitabu changu cha kwanza nitakacho kizindua mapema mwaka 2018. Mafunzo yaliyopatikana katika hadithi hizo fupi za kusisimua ni zipi? Je, wewe umejifunza nini?
Masomo ya thamani zaidi unapaswa kuja na kutoka kwa hadithi hizi za mafanikio ni:
- Kukataliwa haipaswi kukufanya ushindwe kuendelea mbele
- Kushindwa sio tatizokabisa
- Watu wanao kukataa hawajui chochote
- Jiamini mwenyewe ndio ufunguo wa mafanikio ya m aisha yako
Kila mtu anandoto ya kutaka kufanikiwa siku moja, lakini kumbuka ndoto ni kama mbegu ya muanzi ya kule nchini China (Chinnese Bamboo Tree) ambao huchukua muda wa miaka 5 kuweza kutoka ardhini, lakini baada tuu ya kutoka ardhini hurefuka urefu wa futi 80 ndani ya wiki sita. Kumbuka ndani ya kipindi chote cha miaka hiyo mitano mbegu za mianzi hiyo huhitaji kuhudumiwa kama mimea mingine kwa kumwagiliwa maji, ipate jua lakutosha na kukingwa dhidi ya mashumbilio ya magonjwa na wadudu. Swali: Je Chinnese Bamboo tree Umekua kwa kipindi cha muda gani?
Miaka 5 au wiki 6?
TOA MAJIBU HAPO CHINI KWA KUKOMENTI.....
..
..
WASASILIANA NASI KUPITIA
Mob No: 0171411775 / 0753033101 / 0715411245
Barua Pepe: isdorykitunda@gmail.com/sirgwaje@gmail.com
Author: Evarist G.I| Expert in IT Field
No comments:
Post a Comment