Wednesday 20 September 2017

Siri 10 za Mafanikio ya Cristiano Ronaldo

Yeye ni mchezaji wa mpira wa miguu ambaye anacheza Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno.
Yeye ni mchezaji wa kwanza kushinda tuzo nne za viatu vya dhahabu barani Ulaya. Alikuwa mchezaji wa gharama kubwa zaidi duniani wakati alipokwenda kutoka Manchester United kwenda Real Madrid mwaka 2009. Yeye ni Cristiano Ronaldo na hizi ni siri zake  10 za mafanikio.



SIRI 10 ZA MAFANIKIO YA KIJASILIAMALI NA UCHEZAJI MPIRA WA CRISTIANO RONALDO 


SIRI#1. JARIBU TU!
Kila mtu katika familia yangu anapenda soka. Naam nakumbuka siku zote nilipokuwa nikicheza mitaani. Siku moja baba yangu alikuja na akaniambia, "Kwa nini huji kucheza katika klabu ninayofanyiakazi?"  Nikasema, "Ndio kwa nini sio?" Nikaanza kucheza kwenye utaratibu huo na nikaanza kwenda kila siku kwa mafunzo na nilipenda, kuwa sehemu ya timu. 

Kila siku nilipokuwa ninafanya mazoezi baba yangu alikua karibu akinisaidia kwa hali na mali nifanikiwe. Vizuri,  mwanzoni nilijihisi nipo tofauti na watoto wengine. Lakini sikufikiri hata siku moja nitakuwa mchezaji wa kulipwa wa timu kama  Manchester United. 

Hata nilipokua katika klabu ya Sporting. Sikufikiri hata siku moja nitakuja kuwa mchezaji wa kulipwa katika vilabu vikubwa kwani nilikuwa ninacheza kujifurahisha tuu.


SIRI#2. KUWA MSHINDANI
Hii ni muhimu sana kwangu. Siku zote mimi ni mchezaji mshindani.Na sio tu ninapokua uwanjani, bali hata ninapokua nyumbani na dada zangu, binamu zangu na hata mama yangu. Siku zote hua ninajaaribu katika hali na mali nishindane kushinda. Ndio jinsi nilivyo na siwezi kubadilika.
Kwasababu ninafanya hivi siku zote hua ninapenda kufanya kitu ninacho kipenda. Nina yapenda maisha yangu, mimi ni mtu mwenye furaha siku zote. Hivyo basi ushindani ni sehemu ya maisha yangu. Kuanzia Medeira hadi Madrid na kule England nilikua hivyo, ushindani ni sehemu ya maisha yangu.


SIRI#3. SIKU ZOTE TAFUTA CHANGAMOTO MPYA


 Mwandishi: Kwanini uliamua kuhama Manchester United kuelekea Real Madrid?
Ninafikiri siku zote kila kitu kina mwanzo na mwisho wake. Kila kitu nilichokifanya pale Manchester ni kushinda karibu kila kitu na hivyo nilijaaribu kutafuta changamoto nyingine seehemu nyingine.

Hiyo ndio sababu iliyonifanya nihame Manchester United na kwenda klabuni Real Madrid, na sio sababu ya pesa bali changamoto mpya. Hali ya hewa tofauti, lugha tofauti, na chakula tofauti.
Na mambo mengi muhimu ambayo ninayohamia ni changamoto kwa sababu nimependa kujiweka katika shinikizo kuona kile ninaweza kufanya.





SIRI#4. JUA KIPAUMBELE CHAKO


Jambo la kwanza na la mhuhimu zaidi kwangu ni mpira wa miguu. Hakuna kitu kingine zaidi ya hapo. Bila shaka kunavitu vingine ninavyo vipenda. Lakini soka ndio kitu pekee nilichojihusisha nacho kwa kipindi kirefu zaidi toka nilipokuwa na umri wa miaka 18. Hivyo basi kitu pekee ninachokipenda zaidi ni Soka lakini ninapenda maonyesho pia. 


SIRI#5. WATU WATAKUHUKUMU


Siku zote watu hawakujui. Sasa jiulize hao watu ni akina nani ambao watakuhukumu wakati hawakujui? Nikweli hichi kitu sikipendi sana lakini natakiwa nijue jinsi ya kuishi katika mazingira ya namna hii. Siwezi kubadilika, hawezi kubadili utu wangu, hauwezi kubadilisha tabia yangu. Siwezi kubadilisha elimu yangu unayoijua. Ninawaheshimu watu lakini bila shaka sikubaliani kwa sababu watu halisi ambao wananijua mimi ni nani ambaye ni Cristiano. Unaelewa? Kwa hiyo siwezi kubadili mawazo ya watu wengine.

Labda wakati mwingineuwanjani huonyesha kitu ambacho watu hawataki au hawapendi lakini hii ni aina yangu ya kufikiri kwa sababu mimi ni mtu mwenye malengo na hua si tabasamu sana  waksababu hua nataka  nizingatie ninachokifanya.

SIRI#6. FANYA KAZI KWA BIDII


Unatakiwa ufanye kazi. Siku zote hua ninajitahidi kufanya kazi kwa bidii sana na hii imenisaidia niwe katika kiwango cha juu kwa miaka mingi sasa. Sio kwasababu ninajiamini tuu bali ni kwasababu ninafanya kazi ya ziada nje ya uwanja. Nilipokuwa na umri wa miaka 12 hivi watu wengi waliniambia ninakipaji kizuri lakini ni mwembamba sana na mwepesi. Niliiweka akilini mwangu nikaamua nifanyie kazi mwili wangu.

Nilijua ninaweza nikabadilisha muonekano wangu kwa kufanya mazoezi zaidi, kujituma na kujiamini, nilijua ninaweza na nilifanikiwa. Nilijua mabadiliko kidogo katika mikono yangu kutaweza kuleta tofauti kubwa ukilinganisha na wachezaji wengine. 
 
Nilifanikiwa kubadilisha mwili wangu, hivyo ninaendelea kufanya mazoezi kila siku na ndio kunanifanyaniwe katika hali nzuri ya kimchezo siku zote. Ninapenda kuendelea kufanya hivyo kwa sababu inanisaidia sana. Sifanyi mazoezi magumuu kila saiku kwasababu ninatakiwa nifanye hivyo bali ni kwasababu ni sehemu ya maisha yangu.


SIRI#7. AMINI KUWA WEWE NI BORA

Kwa mimi katika akili yangu ninamini mimi ndiye bora zaidi. Kama hufikiri kwa namna hiyo, huishi ubinadamu wako, kama wewe ni mfanya kazi na huamini wewe ni bora, kama wewe ni mkurugenzi wa kampuni ya NIKE, kama wewe ni mwandishi wa makala na hujiamini kuwa wewe ni bora, basi maana yake ni kuwa wewe hauna malengo katika maisha yako. Mimi ninajiamini kuwa  ni bora katika sehemu yangu ninayofanya kazi, hata kama watu wenginehawataki kuamini hilo lakini kiukweli mimi bora akilini mwangu naninamini hivyo.




 



SIRI#8. KUWA SEHEMU YA TIMU


Hakuna, sifuri. Ninajitahidi kufanya vizuri zaidi kila msimu  kushinda kiatu cha dhahabu. Ni muhimu kwangu, na ni kitu ambacho natarajia. Ninawashukuru wachezaji wenzangu kwa sababu wao hunisaidia sana huwa wananipa pasi nzuri ambazo huniwezesha kufunga magoli mengi.

Lakini unajua kile ninachosema nitabadilisha mafanikio yangu binafsi kuwa ya pamoja kama vile katika ligi ya mabingwa au La Liga kwa sababu ni muhimu zaidi. Lakini kwa upande wa wangu binafsi nadhani nitacheza vizuri sana kila msimu na hiyo ndiy
o furaha yangu.


 SIRI#9.  FURAHIA MAISHA YAKO

Amini na fuata ndoto zako. Fanya kazi kwa bidii. Watu wa muhimu zaidi kama vile baba na mama hutarajia mambo mazuri kutoka kwangu hivyo unatakiwa uwaheshimu na uwape furaha ya kweli. Kama unataka uheshimiwe unatakiwa uhishimu watu wengine. Hivi ndivyo hufanya siku zote, kama unanijua unaweza ukaona kwa muda wa miaka sita iliyopita nimeweza kufanya hivyo n ilivyosema hapo juu. 

Nitajibidisha kwa nguvu zangu zote na ikiwezekana hata katika hali ya maumivu ili kufikia malengo yangu zaidi na zaidi. 





SIRI#10. TOA MSAADA


Muda mwingine iliuzidi kufanikiwa zaidi unatakiwa  utoe msaada. Nimekua nikitoa msaada kwa watu wengi hii ni kitu ninachokipenda kwasababu binadamu wote tunahitaji kupeana msaada iili tuwe na furaha ya kweli. Msaada wa kweli sio kuchangia pesa tuu lakini kutembelea wahitaji na kuwafiri ni msaada mkubwa sana ambao ninauishi na ninauheshimu.
  


Thank you very much for being part of our site. 

Author: Evarist G.I| Expert in IT Field  
 
WASASILIANA NASI KUPITIA

Mob No: 0171411775 / 0753033101 / 0715411245

Barua Pepe: isdorykitunda@gmail.com/sirgwaje@gmail.com


THANKS FOR VISITING US!
SHARE TO YOUR FRIENDS 
&

DON'T FORGET TO COMMENT & SHARE  BELOW

"I am living a dream I never want to wake up from. 
CR7 "

No comments:

Post a Comment