Kuna muda watu wamekua wakishindwa kufanikiwa au kusonga mbele katika jambo lolote lile katika maisha. Mambo hayo hua yanaandamana na mambo kadha wa kadha kama vile sina mtaji au nimezeeka au sinasura nzuri nk. Kwa ufupi kabisa unaweza ukazijua aina ya sababu zinazomfanya mtu asiwe na malengo pia asiwe na uthubutu katika jambo lolote lile.
HIZI ni Kauli 10 za mtu asiye na MALENGO wala UTHUBUTU
1. Sina mtaji - Mtaji sio pesa tuu malengo (ideas) ndio mtaji mkuu namba moja. Unaweza ukamuuliza mtu hivi je nikikupa mtaji wa milioni hamsini utafanyia nini? Aina ya majibu unayoweza kuyapata ni kama
@subiri nifikiri ntakupa jibu
@nitafanya biashara
@nitafungua kampuni .
Lakini kiukweli hawa watu wa aina hii hua hawajui ni nini wanataka kufanya. huwa wanatafuta visingizio vya mtaji ili waonekane wanamalengo sema tuu kutokua na pesa kunawasababisha washindwe.
"idea is new money "
2. Sina Connection - Kwani connection inatafutwa au inakutafuta? Watu wa aina hii hua hawaishiwi sababu utaskia wakisema me nimeshindwa kufungua biashara sababu sina connection. Au tujaaribu kuangalia maana ya connection kutoka katika kamusi yakinifu ya Oxford ya Uingereza
What is connection?
A relationship in which a person, thing, or idea is linked or associated with something else.
Maana yake nini hapo: Huyu mtu anasema hana connection akimaanisha hana watu ambao wanaweza wakamshika mkono pale ambapo hatakua na ujuzi au uwezo wa kufanya baadhi ya mambo. Lakini ukweli ni kwamba maana ya connection ni zaidi ya hapo kutoka katika kamusi ya Oxford inatumbia huyu mtu hana watu ambao inaweza ikawa kweli lakini pia hana IDEA wala ELIMU ya kitu anachotaka kukifanya. Hivyo connection ni mjumuisho wa muda, malengo na elimu ya biashara/kazi.
3. Nitaanza rasmi kesho - Watu wa aina hii hua wanajifanya wanamkataba na mungu kua kesho ni lazima ifike. Wanasahau maneno ya wahenga yanayosema:
"Linalowezekana leo usingoje kesho"
Siku zote muda huanza alafu pesa hufuata yani kama ile isemavyo maji hufuata mkondo wake, mkondo huanza alafu maji hufuata nyuma. Hivyo ukiona mtu anayesema atafanya kesho au ataanza kesho basi ujue mtu huyu hana malengo ya kweli wala uthubutu katika jambo lolote lile.
4. Mimi ni wa hivihivi tu - Aina hii ya watu hua inaniacha hoi 😅😅😅 utawasikiwa wakisema:
@umasikini ndio asili yetu
@Ndio jinsi nilivyo we niache tuu
@Pia husema walio fanikiwa wamependelewa
@Mungu ndio alivyonipangia
5. Mifumo mibovu ya Serikali ndiyo inayonirudisha nyuma - Kuna wazazi wasomi na wasio wasomi utawasikia wakisema mfumo wa serikali yetu ndio chanzo cha matatizo au kunifanya niwe maskini.
Wanafunzi nao huko mashuleni hua hawakai kimya utawasikia nao ooh mtaala wa elimu ni mbovu kwa sababu ya mifumo mibovu ya serikali ndio maana tunafeli.
Unaweza ukajiuliza kunawatu wana maisha mazuri sanaa kwa kazi ya kulima kilimo cha mboga mboga tuu ndani ya nchi yenye mfumo mbaya, Je, wewe unashindwa nini? au ukitaka ukitaka ucheke upasuke mbavu zako jaaribu uwaulize ni serikali ipi yenye mfumo mzuri wa kukuwekea pesa mfukoni? Utaskia Marekani au Libya.
Wale wanafunzi wa Tanzania hakuna mfumo wa elimu wa kukuingizia akili kichwani unatakiwa ufanye kazi nzito kusoma kwa bidii ili uweze kufaulu kama wachache wanao faulu mitihani. Serikali inaweza ikawa na mapungufu kama jinsi mtu mmoja mmoja anavyoweza kua na mapungufu ya kuisingizia serikali kua ndio chanzo cha umaskini wake binafsi bila kukumbcajiri ndani yake.
6. Mke/mme/ndugu zangu Ndiyo walioniangusha/kunitenda/kikwazo - Watu wa aina hii hupendelea sana kulalamika na kuwashushia ndugu jamaa na marafiki lawama za kushindwa kwao katika maisha. Kunasheria moja ya huko ughaibu isemayo:
Rule #1 for Success: Do not blame
Kulalamika hata siku moja hakunauwezo wa kubadilisha matokeo ya siku zilizopita, kikubwa ni kujifunza kutokana na makosa na kuangalia ni jinsi gani unaweza ukazaliwa upya katika ulimwengu wa mafanikio. Watu wengi walio fanikiwa hua hawatumii muda wao mwingi kulalamika bali hutumia muda wao mwingi kujua ni jinsi gani watakua na uwezo wa kutatua matatizo ya watu na kujiongezea kipato zaidi na zaidi.
7. Kupata ni majaliwa - Hawa watu hua anadhani maisha ni mchezo wa kamali au bahati nasibu. Utakuta mtu amekaa anacheza draft siku nzima hana mbele wala nyuma afu utamsikia akisema eti kupata ni majaliwa khaa!!! Kweli? Yani Bill Gates hadi anakua mtu tajiri zaidi duniani ni kwasababu ya majaliwa?
"Success is not an accident game like gambling- Evarist G.I"
Ukitaka uyapate majaliwa unatakiwa ufanye kazi kwa bidii ili ndoto yako iweze kufanikiwa. Ogopa sana watu wa aina hii hata kama wanajua nini cha kufanya husubiri majaliwa yao yaje ndio wafanye na ndi kundi linaloongoza kwa kuwa maskini.
..
9. Kuna watu special siyo mimi - Mungu alituumba binadamu bila upendeleo wa aina yoyote ule ndio maana wote tukifundishwa darasani au kazi wote tunauwezo wa kuelewa kinachotofautisha ni kitu kidogo tuu - mmoja ataelewa upesi mwingine ataelewa baadae lakini mwisho wa siku wote tutaelewa tuu. Ukikaa vijiweni utawasikia watu hawa wakisema ooh unamuona CR7 wa Real Madrid yule jamaa najua sana ni special. Ngoja niwaulize haya maswali afu utaona majibuu yao chini:
@Kwani CR7 anamiguu nane?
-Hapana
10. Sina bahati - Watu wengi husahau kuwa kitendo cha kuzaliwa tuu hapa duniani ni ushahidi tosha kua binadamu wote tuna bahati. Kunamsemo mmoja naupenda sana bwana ET - Erick Thomas hupenda kuutumia.
"Luck is last option Dying"
Msemo huu unamaanisha kuwa unapokaribia kushindwa kabisa basi ndio usubiriw hiyo bahati. Lakini bahati hua inatengenezwa. Ukifanikiwa kumuuliza Bill Gates nini siri ya mafanikio yako atakwambia alifanya kazi kwa bidii, aliheshimu ndoto zake na hakukata tamaa, hata siku moja hutokuja kumskia akisema alibahatika kuwa tajiri wa dunia.
Bonus!!!
- Kupata si uhodari nami nitapata tu.
- Mimi ni fungu la kukosa tu.
- Muda wangu bado nitapata tu
- Mungu hajapanga hata vidole mkononi havilingani.
- Wapo waliopangiwa sisi wasindikizaji
- Familia yetu hakuna tajiri nianze mimi?
- Hata wanaotafuta mbona wapo vilevile...fulani namjua mbona yupo tu kama mimi au namzidi.
- Rais anabana sana
*USIFUNGAMANE NA MTU WA AINA HII*
Thank you very much for being part of our site.
Author: Evarist G.I| Expert in IT Field
Credit: Post in whatsapp group
WASASILIANA NASI KUPITIA
Mob No: 0715411245
Barua Pepe: sirgwaje@gmail.com
THANKS FOR VISITING US!
SHARE TO YOUR FRIENDS
&
DON'T FORGET TO COMMENT & SHARE BELOW
No comments:
Post a Comment