Friday 25 August 2017

Jifunze Njia 10 za Kumchepuka Mkeo



Kudanganya mke au msichana wako si kazi rahisi. Ingekuwa hivyo, basi kila mtu angekuwa akifanya hivyo. Jambo hili linaonekana kuwa halina maadili na wengi najua watashangaa kwanini nimeamua kuandika makala hii.

Lakini bado, suala linasimama palepale,  kila aina ya watu hudanganya kwa rafiki zao wa kike, lakini wengi wao hukamatwa mapema au baadaye. Kuna aina ya wanaume ambao wao huchepuka mara moja au mara mbili tuu kisha huacha na hawarudii tena kitendo hicho. Pia kuna watu ambao huchepuka muda wote na wengine hawajawahi kuchepuka kabisa na hawana mpango wowote ule wa kuchepuka. Ikiwa wewe ndio mtu ambaye huchepuki kamwe, makala hii haikuhusu. 

Ikiwa wewe ni mwanaume unayechepuka, unapaswa kusoma makala hii vizuri kwa sababu ikiwa utafanya mambo haya yote 10 vizuri, hutaweza kukamatwa na utaweza kubaki katika uhusiano wako kwa  muda mrefu huku ukujivinjari na mchepuko muda huo huo. 

Unasubiri nini sasa? Soma kwa makini na uchepuke kwa furaha.

Hapa kuna njia 10 za  kumchepuka mpenzi wako.


10. Kuwa na Marafiki watakao danganya kwa ajili yako
 Hii ni muhimu sana. Kuwa na marafiki ambao watadanganya kwa ajili yako inakua ni nzuri kama dhahabu. Kusema kweli katika hali hii unakuwa kama kinga ya bomu la nyuklia. Hebu tuseme unataka kwenda kuchepuka na binti usiku fulani, lakini huwezi kuondoka nyumbani, au labda unataka kumchukua kwenye likizo ya kimapenzi lakini huwezi kwa sababu ya mkeo/mpenzi. Yote hayo ni rahisi ikiwa una rafiki ambao hua wanadanganya kwa ajili yako. Jambo ambalo unatakiwa kufanya ni kumpigia simu rafiki yako na kumwambia aongee na shemeji yake na kumweleza kua atakua na wewe nyumbani kwake mkicheza gemu au mkiona muvi fulani fulani au mtakua na safari ya kwenda kutembelea sehemu za maonyesho ambazo zipo mbali. Hakikisha tuu unarudi kwa wakati muda ule atakapo kuhitaji.


9. Daima Hakikisha Unazima Kompyuta yako
Hii inaonekana kuwa rahisi, lakini ni ajabu jinsi watu wengi hukamatwa tu kwa sababu ya jambo hili rahisi. Daima, na ninamaanisha daima, hakikisha kuwa unaizima  kompyuta yako kila unapomaliza kuitumia. Unatakiwa ufunge barua pepe yako, mitandao yote ya kijamii, na kila kitu ambacho kina mambo yako ya siri. Unaweza hata kufikiri kuwa akaunti yako fulani ipo sawa, lakini labda umesema kitu kidogo katika mazungumzo na binti mmoja huko Facebook ambayo yanaashiria unamahusiano yenye utata. Wakati wanawake wanapohisi, hupitia kompyuta yako na simu yako, mambo ya kwanza wanayojaribu kufanya ni kuangalia historia ya mambo uliyotoka kuyafanya kwenye simu au komputa yako, kwanini aajiri mpelelezi wa siri? Hakikisha unafuta historia ya mambo yote uliyofanya kwenye simu na kompyuta ili usimpe nafasi mpelelezi huyo wa kujitegemea apate taarifa yenye utata.


8. Boresha Mchezo Wako
Kumdanganya mkeo/mpenzi wako kunahitaji majaribio mengi. Wakati unapoanza kufanya hivyo, huenda hautakuwa mzuri sana. Kuwa mchepukaji mzuri ni kama kuendesha baiskeli, unachotakiwa tu usiache, endelea, na kila kitu kitakuwa vizuri. Mwanzo siku zote hua mgumu sana na unapoanza kuchepuka unaweza kujikuta unapoteza rafiki zako wa kike lakini baada ya muda utajikuata unaweza kuchepuka na mpenzi wako wa kike asijue kinachoendelea. Unachotakiwa ukumbuke zaidi kuliko kitu chochote ni kutokukata tamaa. Najua utakuwa na wakati mgumu muda mwingine lakini  muda sio mrefu utajikuta umekua mchepukaji hodari ambaye unauwezo wa kuchepuka na rafiki wa mpenzi wako bila mpenzi wako kujua.

7. Kuwa na Anwani ya barua pepe  kwa ajili ya kudanganya tu.
Kutumia barua pepe yako ya mara kwa mara kumuandikia ujumbe mchepuko wako ni jambo la hatari sana. Unatakiwa utengeneze akaunti feki kwa ajili ya mahusiano ya siri pekee. Ni hatari zaidi hasa pale unapokua na mahusiano na mfanyakazi mwenzako. Wanawake hupenda kujiridhisha kwa wanaume wao kwa kuangalia na kusoma meseji zilizopo kwenye simu na kwenye barua pepe, hivyo basi ukiwa na akaunti feki hatakua na uwezo wa kukuta  kitu. Kumbuka wanawake ni wajanja sana na hujua kuzitumia hisia zao kutaka kujua ukweli wa mambo, basi hutakiwi umpe nafasi ya kujua jambo lolote lile kupitia akaunti yako ya barua pepe.


6. Kaa Mbali na Wafanyakazi Wenzako wa Kike
Najua, wengi mtakubaliana na mimi kuwa na mchepuko sehemu yako ya kazi ni kitu chenye hisia yake ya ajabu na nzuri isiyosimulika.Inakua ni jambo rahisi,  kabisa, kwa sababu unapaswa kuwa kwenye kazi, kwa hiyo ni vigumu sana kwa mpenzi wako kugundua au kuwa na wasiwasi kwani anajua kuwa ni mahusiano ya kikazi. Hisia hii hukufanya uone sehemu ya kazi kuwa ni nzuri zaidi. Tatizo hapa ni kwamba mambo hayo huwa  hayadumu milele, kuna wambea wengi ambao wanaweza kupeleka taarifa kwa mkeo au ikiwezekana hata kuwapiga picha kutunza ushahidi...hiki ni kizazi cha digitali bana.., na ikiwa itaisha vibaya, basi ana uwezo wa kukuharibia kazi yako na Labda hata ndoa yako. Kimsingi, huwezi kujificha kutoka kwa hili, kwa hiyo jitahidi ufanye siri japo kwa muda na ukiona dalili ya kushtukiwa achana nae mapema.  


5. Ficha Simu yako
Najua unaweza kufunga simu yako, bila shaka, na hilo ni jambo zuri. Lakini vipi ikiwa utasahau kuifunga, au utafanya nini ikiwa utaiacha tu wakati unaenda kuoga bafuni? Jambo la msingi hapa ni kuhakikisha simu yako haiondoki usoni mwako kwa namna yoyote ile. Ikitokea umelala usiku basi hakikisha umeizima  simu yako au umezima mlio endapo itapigwa muda wowote basi isisikike. Muda mwingine unatakiwa uwe mbabe tuu, mwanamke mwenye tabia ya kuangalia simu yako muda wote hua ni kero kubwa na muda mwingine anaweza akakuharibia kazi au kukugombanisha na watu wengine akihisi ni michepuko yako. Siri ya mchezo ni kumkatalia asishike simu yako kabisa kwa kisingizio atakuharibia kazi zako lakini chini ya kapeti unafanya mambo yako.

 


4. Usilete Mchepuko wako Nyumbani
Kwa aina fulani ya wanaume, ni furaha ya kumleta mchepuko nyumbani. Najua kwamba hii inaweza kuonekana kuwa ni hatari kwa wengi wenu, lakini hebu tuwe waaminifu. Siko hapa kuhukumu; Mimi niko hapa kukuzuia kupata majanga. Kushiriki mapenzi na mchepuko wako ndani ya nyumba au kitanda unacholalia na mkeo ni jambo ambalo halitakuacha huru hata kidogo, mchepuko wako atakua na uhuru wa kufanya lolote jambo kwa sababu atajiona anapendwa zaidi kuliko hata mkeo na hapo ndio chanzo cha dharau huanza. Mfano asilia ni kwa wanaume wanaopenda kutembea na wafanyakazi wao wa ndani, hukosea kuchepuka kwa kutumia kitanda ambacho hulalia na mkewe kosa linalomfanya mfanyakazi wa ndani avimbe kichwa na kujiona na yeye ni mke wa 2. Dharau huanza na kufanya mama mwenye nyumba kustuka mapema kabisa.



3. Ficha Dhana Zako
Wachepukaji wengi hujifanya wanawapenda wake zao hivyo hutumia kondomu kama kisingizio cha upendo wao kwa wake zao, eti wasiwapelekee magonjwa ya zinaa mmmh!!! Onyo kama unamahusiano ya namna hiyo tafadhali sana hakikisha unazificha katika mazingira ambayo hata mpelelezi wa kutoka FBI au CIA wa marekani hatoweza kuziona, wengi wenu mtajiuliza ni kwanini basi? Mahusiano yamke na mume mara
 nyingi kutumia kinga hua ni jambo lla nadra sana au halipo kabisa, sasa ikitokea umebainika auumekutwa na dhana hiyo ya kujikinga basi maswali mengi yatazuka kama kimbunga cha KATRINA .. uklikua unatumia na nani?  unachepuka na nani? na maswali mengi tatanishi ambayo yatahatarissha ndoa yako amini usiamini usijaaribu kuhifadhi kinga zako kwenye pochi lako la pesa.


2. Zidisha Ustadi Chumbani
Mwanzo wa mahusiano ya mke na mume au wachumba hua ni yakiwango cha juu sana. Muda unavyozidi kwenda kero za hapa na pale hutokea zinazo mpelekea mwanamme aanze tabia za kuchepuka kwa sababu ya kutopata ladha alikyokua akiipata mwanzo kutoka kwa  mkewe au mchumba wake. Lakini makala hii inawazungumzia wanaume wenye tabia za kuchepuka hovyo. Ukishaanza kuchepuka kitu muhimu cha kuzingatia ni kujitahidi kuwa mbunifu zaidi mnapokutana katika tendo la ndoa, wengi hua wanakosea sana pale ambapo wakitoka kuchepuka hurudi nyumbani wakiwa hoi kama mlevi aliyekunywa kreti sita za bia, wakifika hulala kama mtu anayekaribia kukata roho. Mwanamke ni mjanja sana na humjua mwanaume aliyechepuka, sasa ili asijue unatakiwa uwe  mbunifu wa hatari kama Cristiano Ronaldo uwanjani yani badilika na tafuta vituvipya vitakavyo mfanya ajihisi yeye ndiye mtamu zaidi kuliko wengine wote duniani. Hapo hata akiambiwa na watu unachepuka amini usiamini hawezi kuwaamini na ataona wanakutaka au wanataka waharibu mahusiano yenu.




1. Usiandike Meseji Muda Wote Mbele Yake
Wanaume wengine ni wajinga sana na hawajui jinsi ya kutofautisha kati ya kuwa nyumbani na mke au mpenzi wa kike na kuwa kazini au nje ya nyumba, muda wote mtu yupo anachati hata kula anasahua akili yake yote ipo kwenye simu yake tuu. Hata angekua hajielewi lazima atahisi kitu ambacho si cha kawaida umetoka kazini masaa 9 bado unarudi nyumbani akili yako yote ipo kwenye simu  muda wote ni lazima atajenga hisia tatanishi ambayo itakufanya ushtukiwa kirahisi sana. Ukitaka uepuke na hili unatakiwa utumie simu yako kwa makini sana usimpe nafasi mkeo ajue nini ukifanyacho. Unapoenda chooni inaweza ikawa sehemu yako ya kijivinjari kwa muda bila yeye kujua unacahokifanya. Kama nilivyo andika huko juu kuwa simu na kompyuta ni sehemu rahisi zaidi kwa mwanamke kujua kama unachepuka au la.



ONYO: Makala hii ni kwa ajili ya kuelimisha tuu, chepuka for your own risk. Baki njia kuu ukimwi bado upo.








Author: TheActiveDreamer
 
 
WASASILIANA NASI KUPITIA
Mob No: 0171411775 / 0753033101 / 0715411245
Barua Pepe: isdorykitunda@gmail.com/sirgwaje@gmail.com
THANKS FOR VISITING US!
SHARE TO YOUR FRIENDS 
&

DON'T FORGET TO COMMENT & SHARE BELOW
 
There are no secrets to success. It is the result of preparation, hard work, and learning from failure. Colin Powell
Read more at: https://www.brainyquote.com/quotes/quotes/c/colinpowel121363.html?src=t_business
There are no secrets to success. It is the result of preparation, hard work, and learning from failure. Colin Powell
Read more at: https://www.brainyquote.com/quotes/quotes/c/colinpowel121363.html?src=t_business
“Lying, stealing, and cheating are commonplace. Joseph B. Wirthlin "


No comments:

Post a Comment