Thursday 31 August 2017

Mambo 10 Usiyojua Kuhusu Alvaro Morata



Álvaro Borja Morata Martín, ni mchezaji raia kutoka Spain na mchezaji mshambuliaji wa klabu ya Chelsea. Alizaliwa ,23 October 1992. Alianza kuchezea timu ya watoto wa Real Madrid, akachezea timu ya wakubwa wa Real Madrid, Juventus na sasa anakichapa katika timu ya Chelsea ya Uingereza.

Na haya ni mambo machache ambayo ungependa uyajue kumhusu Alvaro Morata.



10. Ni Golikipa Mzuri
Mwaka jana mwezi wa 10 Alvaro Morata alifanya mambo makubwa akicheza kama golikipa alipokuwa mazoezini, aliweza kuokoa michomo ya mbali aliyokuwa akipigiwa na wachezaji wenzake wa timu ya Taifa, huku akiangaliwa kwa umakini na golikipa De Gea.



9. Ni Mfungaji Mzuri
Ukiachana na kuwa golikipa bora Alvaro Morata ni kati ya wafungaji bora kabisa duniani. Akiwa Madrid katika timu ya Watoto aliweza kufanya vizuri sanaa kwa kuchukua tuzo kadhaa za mfungaji bora, piaa mewahi kuwa mfungaji bora kwenye timu ya taifa ya Spain ya vijana chini ya Umri wa miaka 21, amefunga goli kadhaa Madrid na Juventus  na sasa anaendeleza moto wake wa ufungaji akiwa katika timu yake mpya ya Chelsea.
8. Sio Msemaji sana mbele za watu
 Hata anapokua na furaha huogopa kuongea hadharani, kama unakumbuka katika shere zilizofanywa na timu ya Real Madrid mwezi Mei baada ya kuchukua ushindi wa La Liga na Ligi ya mabingwa ulaya alipewa kipaza sauti na ronaldo ili aweze kuongea na mashabiki lakini alikimbia na kujificha iliasiongee.


7.Ana Urafiki wa karibu sana na Sergio Ramos
Mara kwa mara Sergio Ramos na Alvaro Morata wamekua wakionekana wakitaniana wanapokua uwanjani wakati wa mazoezi au hata wanapokua katika vyumba vya kubadilishia nguo. Muda mwingine huonekana wakipigana buti kama sehemu ya kuonyesha urafiki wao, pia jambo la kuchekesha zaidi ni pale ambapo Raamos alimpiga buti Morata alafu Morata akanyanyuka na kuvua suruali akimuonyesha matako Ramos. Morata anakili msaada wa Ramos katika timu ya Taifa na Real Madrid pale anapo muita Ramos kama kiongozi wa kweli uwanjani.



6. Amevunja Rekodi  Akitokea Sabu
Kama unakumbuka katika finali za klabu bingwa ya dunia dhidi ya klabu kutoka Japan ya Kashima Antlers alipoingia kipindi cha pili cha dakika za nyongeza na kuvunja kuwa mchezaji wa kwanza kuingia kama sabu ya nne.

Fifa walifanya jaribio la kwanza la kutoa sabu ya nne pale timu zinapoenda katika hatua ya dakika 30 za nyogeza, na Alvaro Morata ndiye alikua mchezaji wa kwanza kuingia kama sabu ya nne pale alipochukua nafasi ya Ronaldo katika dakika ya 112.



5. Anaipenda Real Madrid sana
Alikili mara kadhaa kuwa anaipenda real Madrid  na hujisikia yupo nyumbani kila anapokua akivaa jezi nyeupe. 

Unakumbuka ile nusu fainali ya klabu bingwa barani ulaya pale Juventus ilipomenyana na Real Madrid? Basi Morata alifunga goli kwa mkwaju wa penalti uliyoipeleka juve katika hatua ya Fainali lakinii katika hali ya kustaajabisha Morata hakuweza kushangilia hata kidogo kuonyesha mapenzi ya timu yake hiyo ya utotoni.





4. Mkewe na Dada yake wote Wanamitindo
Kwa sasa najua unaweza ukawa um=namjua mke wa Morata Alice Campello aliyefunga naye ndoa mwaka jana, akiwa katika fungate katika hali isyo ya kawaida mashabiki wa Man U walikuwa wengi kama ishara ya kumshawishi ahamie klabuni kwao. Alice Campello ni mwanamitindo aliyefanikiwa sana na anawafuasi zaidi ya milioni moja katika akaunti yake ya Instagram. 
Kwa wale wachache tuu ndio wanajua kama dada yake Marta Abril Morata Martin ana wafuasi 66,000 katika akaunti ya Instagram. 



3. Anajua kutunza na kutekeleza Ahadi
Alipotembelea hospital moja pale mjini Madrid Machi 2014 aliwaahidi watoto walioathirika na kansa kuwa atanyoa nywele kama wao ilikuonyesha heshima na utu. Alifanya kama alivyo ahidi dhidi ya mechi dhidi ya Rayo Vallecano.  Kiukweli anajua jinsi ya kukamilisha ahadi zake na pia alifunga goli moja katika ushindi wa goli 4-0.



2. Pesa sio kila kitu kwake
Aliweza kukataa pesa nyingi sana pale alipopewa ofa ya kuhamia katika ligi ya China dau lenye thamani ya Euro 147 milioni, na mshara wa thamani ya paundi milioni 29.4 kutoka kwenye Chinese Super League lakini alikataa na sasa yupo Samford Bridge.



1. Gari lake la kwanza kumiliki na Volkswagen Golf


MAKALA IJAYO  ZIJUE GARI 10 ANAZO MILIKI CR7
USIKOSE


WASASILIANA NASI KUPITIA
Mob No: 0171411775 / 0753033101 / 0715411245
Barua Pepe: isdorykitunda@gmail.com/sirgwaje@gmail.com

Author: Evarist G.I| Expert in IT Field
 

THANKS FOR VISITING US!
SHARE TO YOUR FRIENDS 
&

DON'T FORGET TO COMMENT & SHARE  BELOW
 
There are no secrets to success. It is the result of preparation, hard work, and learning from failure. Colin Powell
Read more at: https://www.brainyquote.com/quotes/quotes/c/colinpowel121363.html?src=t_business
There are no secrets to success. It is the result of preparation, hard work, and learning from failure. Colin Powell
Read more at: https://www.brainyquote.com/quotes/quotes/c/colinpowel121363.html?src=t_business
"Any man who reads too much and uses his own brain too little falls into lazy habits of thinking. Albert Einstein "

No comments:

Post a Comment